VIGEZO vya kupata Mikopo ya Halmashauri

VIGEZO vya kupata Mikopo ya Halmashauri
VIGEZO vya kupata Mikopo ya Halmashauri

Utaratibu na Vigezo vya Kupata Mikopo ya asilimia kumi itolewayo na Halmashauri, Mikopo ya halmashauri kwa vijana 2024.

MIKOPO YA 10% KUTUMIA MFUMO WA WEZESHA PORTAL

Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imesanifu na kujenga Mfumo wa Wezesha Portal utakaotumika kukopesha mikopo ya asilimia 10, mikopohalmashauri.tamisemi.go.tz

VIGEZO na Taratibu za Kupata Mikopo ya Kundi la Wanawake na Vijana
  • Kikundi lazima kisajiliwe kama kikundi cha wanawake au vijana.
  • Kikundi cha wanawake au vijana kiwe kinajishughulisha na ujasiliamali au kinakusudia kuanzisha shughuli za ujasilamali mdogo au wa kati.
  • Kwa kikundi cha wanawake au vijana kiwe na idadi ya wanakikundi kuanzia watano na kuendelea.
  • Kikundi cha wanawake au vijana lazima kiwe na akaunti ya benki ya iliyofunguliwa kwa jina la kikundi na kwa ajili ya matumizi ya kikundi.
  • Kikundi cha wanawake/vijana lazima wawe raia wa Tanzania wenye akili timamu na umri wa miaka 18 na kuendelea.
  • Kwa vikundi vya vijana lazima umri uzingatiwe kuanzia miaka 18 na ukomo wake ni miaka 35.
  • Wanufaika wa mikopo hii ni wale wasio na ajira rasmi.
  • Vikundi vyote lazima viwe na barua toka kwa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa kwamba kikundi husika anakitambua kwa upana na miradi ya kikundi ilipo.
  • Kikundi cha wanawake/vijana wanaojishughulisha na biashara lazima wawe na leseni  ya kikundi.
  • Kikundi cha wanawake/vijana lazima kila mwanachama awe na kitambulisho cha NIDA
VIGEZO na Taratibu za Kupata Mikopo ya Kundi la Watu wenye Ulemavu
  • Kundi hili linaweza kukopeshwa kikundi au mtu mmoja,endepo Kamati ya kudumu ya Fedha,Mipango na Uongozi itajiridhisha kuwa mtu huyo amekosa mtu mwingine mwenye ulemavu na sifa ya kuwa mwanakikundi wa kikundi cha watu wenye ulemavu.
  • Anajishughulisha na ujasiriamali au anakusudia kuanzisha shughuli za ujasiriamali mdogo au wa kati.
  • Mlemavu lazima awe na akaunti benki  yenye jina lake halisi kwa matumizi yake ya kijasiriamali
  • Awe raia wa Tanzania mwenye akili timamu na umri wa miaka 18 na kuendelea.
  • Wanufaika wa mikopo hii ni wale wasio na ajira rasmi.
  • Kwa mtu mmoja mlemavu anayeomba mkopo lazima awe na cheti cha kuzaliwa.
  • Kwa kikundi/Mlemavu mmoja  lazima kuwa na barua toka kwa Mtendaji wa Kijiji/Mtaa kwamba kikundi husika anakitambua kwa upana na miradi ya kikundi ilipo.
  • Kikundi cha watu  wenye ulemavu/Mtu mwenye ulemavu anayejishughulisha na biashara lazima wawe na  Leseni ya biashara.
BONYEZA HAPA KUANZIA MKOPO WA ASILIMIA 10 KWA HALMASHAURI MBALIMBALI.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA