UFAHAMU Mfumo wa ESS Utumishi - ESS.utumishi.go.tz

UFAHAMU Mfumo wa ESS Utumishi - ESS.utumishi.go.tz
UFAHAMU Mfumo wa ESS Utumishi - ESS.utumishi.go.tz

ESS Utumishi ni mfumo wa kidijitali, unalomilikiwa na Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unaolenga kuboresha utoaji wa huduma kwa watumishi wa umma nchini Tanzania.

Kupitia mfumo huu Watumishi wa Umma wanaweza kupata taarifa zao za kibinafsi, mishahara, na kushughulikia mchakato wa uhamisho kwa urahisi zaidi.

Mfumo huu umepunguza urasimu wa makaratasi na kuongeza ufanisi katika sekta ya umma, Watumishi wa umma wanashauriwa kutumia kikamilifu mfumo huu kwa manufaa ya kazi zao.

ESS Utumishi (Watumishi Portal) - Kupitia Makala hii tumekuwekea muongozo wa jinsi ya kuingia na kutumia mfumo wa (ESS Utumishi, faida zake, na huduma mbalimbali zinazotolewa na mfumo huo.

Kwa kutumia ESS Utumishi, Watumishi wa Umma wanaweza kuona taarifa zao binafsi kama mishahara, na rekodi za huduma, na vilevile kushughulikia mchakato wa uhamisho kutoka eneo moja hadi jingine au mkoa mmoja hadi mwingine.


Jinsi ya Kuingia Kwenye ESS Utumishi - Watumishi Portal


Ili kuingia kwenye mfumo wa ESS Utumishi, fuata hatua hizi;

  • Tembelea kiungo link hii: https://ess.utumishi.go.tz
  • Ingia na taarifa zako, ambazo ni jina lako la mtumiaji (check number) na nywila/neno la siri.
  • Baada ya kuweka taarifa zako, bonyeza kitufe cha “Login” ili kuingia kwenye akaunti yako.
  • Kama umesahau nywila yako, bonyeza neno “Reset Password?” ili kurejesha nywila yako.
  • Ingiza jina lako la mtumiaji ambalo ni namba yako ya utumishi (check number).
  • Utapokea maelekezo kupitia barua pepe au SMS
  • Fuata maelekezo kwenye uliyopewa na ingiza nywila mpya unayotaka kutumia kwa mfumo huo wa ESS Utumishi.
Jinsi ya Kujisajili Kwenye ESS Utumishi - Watumishi Portal
  • Kama wewe ni mtumishi mpya na hujajiandikisha, bonyeza kiungo cha “Click here to register” ili kujiandikisha kwenye mfumo huo na endelea na utaratibu mwingine baada ya kukamilisha usajili.

UFAHAMU Mfumo wa ESS Utumishi - ESS.utumishi.go.tz
Mfumo wa ESS Utumishi ulianzishwa kwa malengo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na;

  • Kuwawezesha watumishi wa umma kupata taarifa zinazohusiana na ajira zao kama vile mishahara na taarifa za binafsi kwa urahisi.
  • Kwa kutumia mfumo huu pia watumishi wa umma wanaweza kuboresha taarifa zao za kibinafsi na kushughulikia mchakato wa huduma kwa ufanisi zaidi bila kutumia makaratasi.
  • ESS Utumishi pia ni njia mbadala ya kisasa ya kushughulikia taarifa za kiutumishi ambayo inapunguza matumizi ya makaratasi na urasimu wa kiofisi.

Hizi hapa ni baadhi ya Faida za Mfumo wa ESS Utumishi


Watumiaji wa mfumo huu ni pamoja na watumishi wote wa umma chini ya serikali ya Tanzania.


Mfumo huu unaleta faida kadhaa kama vile:

  • Upatikanaji wa taarifa binafsi - Mfumo una interface rahisi ambayo inawawezesha watumiaji kuangalia taarifa zao za ajira bila ugumu.
  • Upatikanaji wa data za mishahara - Mfumo unawawezesha Watumishi wa Umma kuona taarifa zao za Mishahara kila mwezi.
  • Usaidizi wa kiufundi - Kuna timu maalum ya usaidizi inayopatikana kusaidia masuala yoyote ya kiufundi yanayotokea.

Mfumo wa ESS Utumishi pia unatoa nafasi kwa watumishi wa umma kuangalia taarifa zao binafsi kama vile jina kamili, tarehe ya kuzaliwa, namba ya utumishi, cheo, na idara wanayofanyia kazi.


Hii inasaidia sana kuhakikisha taarifa zilizopo kwenye mfumo ni sahihi, na pale inapohitajika, Mtumishi anaweza kusasisha taarifa zake.


Kupitia Mfumo wa ESS Utumishi, Watumishi wa Umma wanaweza kupata taarifa zao za mishahara moja kwa moja kutoka kwenye mfumo wa ESS Utumishi.


Hii inajumuisha kiasi cha mshahara wa mwezi, makato ya kodi, na michango mingine. Mfumo huu una faida kwa kuwa watumishi wanaweza kufuatilia mabadiliko yoyote kwenye malipo yao ya kila mwezi.


Mfumo wa ESS Utumishi pia unawawezesha Watumishi wa Umma kushughulikia mchakato wa uhamisho wa kituo cha kazi.


Mtumishi anaweza kutuma maombi ya kuhamishwa kutoka taasisi moja kwenda nyingine au kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine moja kwa moja kupitia mfumo huu.


Hii inarahisisha mchakato wa uhamisho ambao awali ulitegemea sana makaratasi na usimamizi wa ofisi.


Mfumo huu pia unatoa matangazo muhimu kwa watumishi wa umma, kama vile taratibu mpya za ajira, mabadiliko ya sheria au kanuni za kiutumishi, na taarifa nyingine zinazohusu watumishi wa umma kwa ujumla.

MAELEKEZO YA NAMNA YA KUTUMIA HUDUMA YA UHAMISHO KWENYE DIRISHA LA WATUMISHI PORTAL KWA VIDEO BONYEZA HAPA.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA