TCU Yaongeza muda Udahili wa Shahada ya Kwanza 2024/2025

TCU Yaongeza muda Udahili wa Shahada ya Kwanza 2024/2025

TCU Yaongeza muda Udahili wa Shahada ya Kwanza 2024/2025

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imeongeza muda wa Udahili wa Shahada ya Kwanza Katika Programu ambazo bado zina Nafasi Kwa Mwaka wa Masomo 2024/2025.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na wadau wa Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi kuwa udahili katika awamu zote mbili kwa ngazi ya Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2024/2025 umekamilika.

Majina ya waliodahiliwa katika Awamu ya Pili yametangazwa na vyuo husika leo tarehe 05 Oktoba, 2024 au unaweza yatazama hapa chini;

Orodha ya waombaji waliodahiliwa zaidi ya Chuo kimoja au Program zaidi ya moja katika awamu ya pili ya udahili na wale ambao hawakuthibitisha awamu zilizopita kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja katika Awamu ya Pili na wale ambao hawakuweza kuthibitisha udahili katika Awamu ya Kwanza, wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 05 hadi 21 Oktoba, 2024.

Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili. 

Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika. 

Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili.

Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja itapatikana kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz) tarehe 05 Oktoba, 2024. 

Baada ya kukamilika kwa awamu zote mbili za udahili, Tume imepokea maombi ya kuongeza muda wa kutuma maombi ya udahili kutoka kwa Jumuiya ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania (TAHLISO), baadhi ya waombaji ambao hawakufanikiwa kupata udahili katika awamu zilizopita na pia vyuo ambavyo bado vina nafasi vimeomba vipewe muda kuendelea kudahili.

Hivyo, Tume imeongeza muda wa udahili kwa kufungua Awamu ya Tatu na ya mwisho ya udahili itakayoanza leo tarehe 05 hadi 09 Oktoba, 2024.

Tume inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Pili kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda. 

Aidha, Tume inaelekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kuendelea kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.

Waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa Awamu ya Tatu kama ilivyoainishwa katika Jedwali.

Jedwali: Utaratibu wa udahili katika awamu ya Tatu kwa mwaka wa masomo 2024/2025.

Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa. 

TCU Jinsi ya Kuthibitisha Udahili

TCU Mwongozo wa Udahili wa Shahada ya Diploma 2024/2025

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA