SIMBA na Yanga Kukutana Algeria December 2024

SIMBA na Yanga Kukutana Algeria December 2024
SIMBA na Yanga Kukutana Algeria December 2024

Kwa mara ya kwanza, timu za Simba na Yanga zitakuwa nchini Algeria kwa wakati mmoja (ndani ya wiki moja) kwenye mechi za michuano ya CAF, kila timu ikiwa na kibarua chake.

Wiki hiyo ni ile yenye tarehe 6-8 December 2024, ambapo Simba itakuwa nchini kucheza mchezo wa raundi ya pili hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho (CAF Confederation Cup 2024/2025) dhidi ya CS Costantine katika mji wa Costantine.

Kwa Upande wa Young Africans wao watakuwa katika Mji wa Algiers kucheza dhidi ya MC Alger, mchezo wa hatua hiyo hiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League 2024/2025).

Mechi hizi huenda zikapishana kwa siku moja hadi mbili lakini pia huenda zikapigwa katika miji tofauti ambayo ni Costantine na Algiers.

Ratiba Kamili ya Simba CAF Confederation Cup 2024/2025 iko hivi:-
28/11/2024: Simba vs Bravos.
08/12/2024: Costantine vs Simba.
15/12/2024: Simba vs Sfaxien.
05/01/2025: Sfaxien vs Simba.
12/01/2025: Bravos vs Simba.
19/01/2025: Simba vs Costantine.

Ratiba kamili ya Yanga CAF Champions League 2024/2025 iko hivi:-
26/11/2024: Yanga vs Al Hilal.
06/12/2024: MC Alger vs Yanga
13/12/2024: TP Mazembe vs Yanga
03/01/2025: Yanga vs TP Mazembe
10/01/2025: Al Hilal vs Yanga
17/01/2025: Yanga vs MC Alger.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA