SENSA ya Watu na Makazi hufanyika baada ya Muda gani?

SENSA ya Watu na Makazi hufanyika baada ya Muda gani?
SENSA ya Watu na Makazi hufanyika baada ya Muda gani?

Serikali ya Awamu ya Sita, imetimiza wajibu wake wa kufanya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kama ilivyofanyika katika Awamu nyingine Tano zilizopita ambapo Sensa hizo zilifanyika katika miaka ya 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012.

Sensa hii imefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Takwimu Sura 351 ambayo inaelekeza Serikali kufanya Sensa ya Watu na Makazi kila baada ya miaka kumi.

Halikadhalika, Sensa imefanyika 
kukidhi matakwa ya kimataifa ambapo Umoja wa Mataifa unazitaka nchi kufanya 
Sensa ya Watu na Makazi angalau mara moja ndani ya miaka kumi.

Sensa ya Mwaka 2022 imefanyika katika kipindi cha utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Umoja wa Mataifa wa kufanya Sensa katika miaka ya 2020 ambao ulianzia mwaka 2015 na utaishia mwaka 2024. 

Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kwaajili ya mipango 
jumuishi na maendeleo endelevu ya nchi na yataongeza uwazi katika kugawa 
rasilimali zilizopo kuendana na uwiano wa idadi ya watu katika ngazi zote za utawala.
 
Halikadhalika matokeo yatatumika na Serikali na wadau wengine katika kufuatilia na kutathmini mipango mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ikijumuisha Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025 na Dira ya Zanzibar 2050, Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Mwaka 2021/22 - 2025/26 na Mpango wa Maendeleo wa Zanzibar (2021/22 - 2025/26), Dira ya Maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki 2050 naAjenda ya Maendeleo ya Afrika 2063.

Taarifa hizi zitaipima Tanzania katika hatua iliyofikia kwenye utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu; Mpango ambao unalenga kuleta usawa na kutokomeza umaskini wa aina zote ukiwemo umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030 kwa kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayeachwa nyuma.

Chapisho la Matokeo ya mwanzo ni la kwanza katika mtiririko wa machapisho 
yaliyopangwa kutolewa kutokana na Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022. 

Dhumuni kuu la kuandaa chapisho hili ni kutangaza jumla ya idadi ya watu 
waliohesabiwa nchini kwa jinsi na kwa mikoa.

Taarifa hii ni muhimu kwa vile 
itajulisha umma hali halisi ya idadi ya watu nchini, Tanzania Bara na Zanzibar na 
kwa kila mkoa.

Aidha, mwenendo wa ongezeko la watu kutoka Sensa ya mwaka 1967 mpaka 2022 umeainishwa.

Chapisho hili litatoa pia jumla ya majengo yote nchini, aina ya majengo na majengo yenye anwani za makazi na huduma za jamii. 

SENSA ya Watu na Makazi hufanyika baada ya Muda gani?

Sensa ya Watu na Makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchakata, kuchambua, 
kutathmini, kuchapisha, kusambaza na kutunza takwimu za kidemografia, kiuchumi na mazingira wanayoishi katika nchi kwa kipindi maalum.

Utaratibu huu huwezesha kupatikana kwa taarifa za msingi za kitakwimu kama idadi ya watu wote kwenye nchi kwa umri, jinsi, hali ya ulemavu, hali ya elimu, shughuli za kiuchumi, hali ya makazi, vizazi, vifo na nyingine kama zilivyoainishwa katika Dodoso la Sensa (Angalia Kiambatisho A).

Dhumuni kuu la kufanya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 ni kupata 
viashiria vya msingi vya watu na makazi ambavyo vitawezesha katika kutunga sera, 
kupanga, kufuatilia mipango ya maendeleo ya kimkakati inayolenga kukuza ustawi 
wa nchi na wananchi. Aidha, matokeo ya Sensa yataiwezesha Serikali na wadau 
wengine kufuatilia na kutathmini malengo yaliyofikiwa katika utekelezaji wa
mipango ya maendeleo iliyokusudiwa kwa lengo la kukuza uchumi na ustawi wa 
jamii na hatimae kupunguza umaskini.

Utofauti wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 na sensa zilizopita umepelekea kuwa na ubora wa hali ya juu wa takwimu za sensa

 Sensa hii imetumia teknolojia ya kidigitali katika utekelezaji wake kuanzia kwenye zoezi la utengaji wa maeneo ya kijiografia ya kuhesabia watu katika ngazi za shehia, mitaa na vitongoji, hadi kwenye zoezi la kuhesabu watu. Matumizi ya vishikwambi (tablets) katika hatua zote za utekelezaji kumesaidia katika kupunguza gharama za uendeshaji, usomaji wa majira nukta katika kaya, majengo, ukusanyaji Taarifa kutoka katika huduma zote za jamii na katika zoezi la kuhesabu watu na hii imechangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha taarifa zilizokusanywa.

Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 
imekusanya taarifa nyingi zaidi ambapo Dodoso Kuu lilikuwa na maswali 100 
ikilinganishwa na sensa ya 2012 ambayo ilikuwa na maswali 64.

Hali hii imesababishwa na mabadiliko makubwa ya kiuchumi duniani pamoja na kuongezeka zaidi kwa matumizi ya teknolojia kulikosababisha uwepo wa mahitaji makubwa ya takwimu nchini.
SENSA ya Watu na Makazi hufanyika baada ya Muda gani?

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilifanya maamuzi ya utekelezaji wa Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi kwa kutumia mfumo wa utekelezaji wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuipunguzia Serikali gharama ya kufanya mazoezi matatu makubwa katika 
vipindi tofauti.

Taarifa za majengo na anwani za makazi ni kielelezo muhimu sana kwa Taifa na kwa mwananchi mmoja mmoja kwa ajili ya makazi na shughuli nyingine muhimu za maendeleo.

Sensa ya Majengo na Anwani za Makazi ni zoezi ambalo limefanyika kwa mara ya kwanza Nchini tangu kuasisiwa kwa muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Taarifa za majengo zilikuwa zinakusanywa 
katika tafiti za kitaifa zilizokuwa zinaganyika kila baada ya miaka mitano kwaajili ya kuboresha sera ya mipango Nchi. 

Taarifa za majengo yote Nchini na anwani za makazi zitaiwezesha Serikali katika 
kuandaa sera, sheria, kanuni za mipango miji na programu mbalimbali za maendeleo katika Taifa.

Halikadhalika, taarifa za majengo na anwani za makazi za mwaka 2022 zitatumika katika kujitathmini kwa miaka ijayo katika uandaaji wa taarifa za 
utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDG) na Agenda 2030 ya Shirika 
la Umoja wa Mataifa la Makazi (UN-Habitat). 

Hata hivyo, uwekaji wa anwani za makazi ni endelevu, hivyo Serikali ya Jamhuri ya 
Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar zitaendelea na zoezi la
uwekaji wa anwani za makazi na ukusanyaji wa taarifa za majengo yote 
yanayotarajiwa kujengwa nchini, ili kuweza kuhuisha kanzidata za majengo na 
anwani za makazi.

MGAWANYO WA WATU
Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaonesha kuwa, idadi ya 
watu nchini imeongezeka kutoka 44,928,923 waliohesabiwa mwaka 2012 hadi kufikia watu 61,741,120 kwa mwaka 2022, sawa na wastani wa ongezeko la idadi ya watu kwa mwaka (the annual intercensal population growth rate) la asilimia 3.2.

Kwa Tanzania Bara, idadi ya watu imeongezeka kutoka 43,625,354 mwaka 2012 hadi watu 59,851,347 mwaka 2022 wakati kwa Tanzania Zanzibar idadi ya watu imeongezeka kutoka 1,303,569 mwaka 2012 hadi watu 1,889,773 mwaka 2022 (Angalia Kielelezo Na. 1)
SOMA ZAIDI TAARIFA HII HAPA
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA