NAFASI 1300 za Kazi Chuo kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)

NAFASI 1300 za Kazi Chuo kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA)
TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA 1300 KUPITIA PROGRAMU MAALUM YA KUENDELEZA ZAO LA PAMBA NCHINI- INARUDIWA

Kwa mara nyingine tena Chuo kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Wizara ya Kilimo katika utekelezaji wa programu ya kushirikisha vijana katika kilimo ya Jenga Kesho Iliyo bora (Building a Better tomorrow- BBT).

BBT inatekelezwa kupitia mikakati na miradi mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa mazao na baadhi ya malengo yake ni kuongeza ajira kwa vijana na wanawake 20,000 kupitia shughuli za kukuza ujuzi (internship), kuanzisha 
shughuli za kiuchumi 12,000 katika ngazi ya vijiji pamoja na kilimo cha mashamba makubwa (Block farms) ifikapo mwaka 2030.

Kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha huduma za ugani hapa nchini, wizara ya kilimo imepanga kutekeleza pia program maalum huduma za ugani kupitia vijana wahitimu (BBT Agricultural Extension Entrepreneurship Scheme- BBT AEES).

Kupitia BBT-AEES nafasi elfu moja
na mia tatu (1300) zinahitajika kujazwa na wahitimu wenye sifa stahiki katika fani za kilimo ili kutoa huduma za ugani katika zao la pamba kwa utaratibu wa ajira za muda kama ifuatavyo:-

✅Nafasi: Afisa kilimo/ (Nafasi 700)

Majukumu ya muhimu ni pamoja na:
Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa 
thamani wa zao la pamba kwa kufanya yafuatayo:
  • Kutoa elimu ya kilimo bora cha pamba kwa wakulima kuanzia kuandaa shamba, kuvuna hadi kuhifadhi ghalani
  • Kutoa elimu na kusimamia ubora wa pamba kuanzia shambani hadi ghalani
  • Kufuatiliia na kuhakikisha kuwa wakulima wanazingatia kanuni za kilimo bora cha pamba
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya kila wiki kuhusu maendeleao ya kilimo katika eneo husika
  • Kuandaa mahitaji ya pembejeo kwa wakulima na kuyawasilisha katika mamlaka husika
  • Kusimamia na kuhakikisha pembejeo zinazopelekwa katika eneo husika zinawafikia wakulima kikamilifu
  • Kusajili wakulima na wadau wengine ikiwemo watoa huduma za pembejeo katika eneo lake kwenye mfumo wa kidijitali uliopo
  • Kutoa mafunzo na kuanzisha vikundi vya wakulima na kuvisimamia
  • Kuanzisha mashamba ya mfano na shamba darasa katika eneo la kazi
  • Kuwatambua wadau wa sekta kilimo waliopo katika eneo la kazi na kuwaunganisha  na wakulima ili kupata huduma wanazotoa
  • Kuhakikisha kila mkulima ana daftari ambalo litatumika kujaza huduma  zitakazotolewa na wadau mbalimbali
  • Kukusanya, kuandaa na kuchakata takwimu za uzalishaji katika eneo lake kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji takwimu (Agricultural Routine Data System (ARDS)
  • Kusimamia matumizi ya mfumo wa kidijitali ya kutoka huduma za ugani na
  • Kutoa ushauri kwa mazao mengine yanayolimwa na wakulima wa kijiji  anachokisimamia
Sifa zinazohitajika
Kwa nafasi hii mwombaji awe na sifa zifuatazo:
  • Awe mtanzania mwaminifu, mweye kujituma na mahusiano mazuri na wengine
  • Awe amehitimu shahada katika fani ya sayansi ya kilimo, Agronomia au uzalishaji  mazao kutoka chuo kinachotambulika na serikali
  • Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma
  • Awe hajawahi kufungwa kwa makossa yoyote ya jinai
  • Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa
  • Awe tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama itakavyoainishwa katika mkataba
  • Awe mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40
  • Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa kipindi cha msimu husika
  • Uzoefu wa kazi katika zao la pamba au ushiriki wa mafunzo ya kukuza ujuzi  (internship) ndani au nje ya nchi ni sifa za ziada
✅Nafasi : Afisa kilimo msaidizi (Nafasi 600)

Majukumu ya muhimu ni pamoja na:
Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa 
thamani wa zao la pamba kwa kufanya yafuatayo
  • Kutoa elimu ya kilimo bora cha pamba kwa wakulima kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna
  • Kutoa elimu na kusimamia ubora wa pamba kuanzia shambani hadi ghalani
  • Kufuatiliia na kuhakikisha kuwa wakulima wanazingatia kanunu za kilimo  bora cha pamba
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya kila wiki kuhusu maendeleao ya kilimo katika  eneo husika
  • Kuandaa mahitaji ya pembejeo kwa wakulima na kuyawasilisha katika  mamlaka husika
  • Kusimamia na kuhakikisha pembejeo zinazopelekwa katika eneo husika  zinawafikia wakulima kikamilifu
  • Kusajili wakulima na wadau wengine ikiwemo watoa huduma za pembejeo katika  eneo lake kwenye mfumo wa kidijitali uliopo
  • Kushiriki katika kuanzisha mashamba ya mfano na shamba darasa katika eneo la kazi
  • Kuwatambua wadau wa sekta kilimo waliopo katika eneo la kazi na kuwaunganisha  na wakulima ili kupata huduma wanazotoa
  • Kufuatilia na kusimamia utunzaji na usimamizi wa daftari la mkulima ambalo  litatumika kujaza huduma zitakazotolewa na wadau mbalimbali
  • Kusaidia kukusanya, kuandaa na kuchakata takwimu za uzalishaji katika eneo lake  kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji takwimu (Agricultural Routine Data System  (ARDS)
  • Kushiriki kusimamia matumizi ya mfumo wa kidijitali ya kutoka huduma za ugani
Sifa zinazohitajika
Kwa nafasi hii mwombaji awe na sifa zifuatazo:
  • Awe mtanzania mwaminifu, mweye kujituma na mahusiano mazuri na wengine
  • Awe amehitimu stashahada katika fani ya sayansi ya kilimo au uzalishaji mazao  kutoka chuo kinachotambulika na serikali
  • Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma
  • Awe hajawahi kufungwa kwa makossa yoyote ya jinai
  • Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa
  • Awe tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama  itakavyoainishwa katika mkataba
  • Awe mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40
  • Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa kipindi cha msimu husika
  • Uzoefu wa kazi katika zao la pamba au ushiriki wa mafunzo ya kukuza ujuzi  (internship) ndani au nje ya nchi ni sifa za ziada
Jinsi ya kutuma Maombi
Maombi yote yaambatane na
vivuli vya vyeti vya kuzaliwa, NIDA, vyeti vya elimu ya sekondari, stashahada na shahada kutoka vyuo vya mafunzo vinavyotambuliwa na serikali. Wahitimu watarajiwa (2024) wenye sifa tajwa hapo juu, wanahamasishwa kutuma maombi yao wakiambatanisha pia nakala za “partial transcript” au “results slips”.

Picha mbili za hivi karibuni za “passport size” za mwombaji

Wasifu (Curriculum vitae) wa mwombaji pamoja na anuani kamili, mawasiliano ya simu, barua pepe na anuani za wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
Maombi yote yatumwe kwa Rasi wa ndaki ya Kilimo ya Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo kupitia barua pepe coahr@sua.ac.tz na nakala kwa mkurugenzi- kurugenzi ya Shahada za awali ya chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo dus@sua.ac.tz.

Waombaji wanashauriwa kutuma maombi 
yao kupitia barua pepe ingawa wanaweza pia kuleta maombi moja kwa moja kwa ofisi tajwa hapo juu.

Maombi yote yawe yametufikia kabla au ifikapo tarehe 13 Oktoba 2024.

Kwa maelezo zaidi au maswali juu ya tangazo hili tafadhali tupigie kupitia namba zifuatazo: +255760485718
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA