Taarifa kwa Umma Kuhusu Kuchelewa Kutoka kwa Matokeo ya Uhakiki wa Wanafunzi kwa awamu ya Pili Kutoka NACTVET.
Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET)
linapenda kutoa taarifa kwa umma kwamba, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wa Baraza matokeo ya uhakiki wa wanafunzi kwa awamu ya pili yaliyotarajiwa kutoka tarehe 2 Oktoba, 2024 yatatoka tarehe 6 Oktoba 2024.
Baraza hilo linaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na
mabadiliko haya.