NACTVET Matokeo ya Uhakiki wa Waombaji Waliochaguliwa Awamu ya Pili 2024/2025

NACTVET Matokeo ya Uhakiki wa Waombaji Waliochaguliwa Awamu ya Pili 2024/2025
NACTVET Matokeo ya Uhakiki wa Waombaji Waliochaguliwa Awamu ya Pili Mkupuo wa Septemba 2024/2025.

Baraza linautaarifu umma kuwa matokeo uhakiki wa awamu ya Pili kwa waombaji waliochaguliwa kujiunga na programu mbalimbali kwa mkupuo wa Septemba, 2024 katika ngazi ya Astashahada na Stashahada yametolewa rasmi tarehe 7 Oktoba, 2024.

Jumla ya waombaji 45,540 kati yao wanawake 21,525 (47%) na wanaume 24,015 (53%) waliwasilishwa kwa ajili ya uhakiki kutoka katika vyuo vilivyokidhi vigezo vya kudahili wanafunzi.

Kati ya waombaji 44,088 (97%) waliokidhi 
vigezo na sifa za kujiunga na programu na wakachaguliwa, wanawake ni 20,722 na wanaume ni 23,366. Waombaji 1,452 (03%) hawakuwa na sifa katika programu walizochaguliwa.

Waombaji wote wanaweza kupata taarifa zao za uhakiki kwa kutumia msimbo uliotumwa kwenye namba ya simu kwa kubonyeza kitufe cha “Uhakiki muhula 
Baraza linawasisitiza waombaji wote kutunza msimbo waliyotumiwa kwani ndio utatumika katika usajili pindi mwombaji atakapofika katika chuo alichokichagua 
kwa ajili ya kuanza masomo. 

Aidha, Baraza linavielekeza vyuo kuwasajili waombaji waliohakikiwa na Baraza na kuonekana wana sifa.

Usajili huo wa wanafunzi watakaofika vyuoni utaanza tarehe 10 Oktoba hadi 30 Novemba, 2024; na utafanyika kwa kutumia misimbo iliyotumwa na Baraza kwenye namba za simu za waombaji.

Chuo kitakachokiuka taratibu za udahili, hatua stahiki zitachukuliwa dhidi ya chuo husika.

Baraza litafungua dirisha la marekebisho kuanzia tarehe 10 hadi 15 Oktoba, 2024 
ili waombaji waliohakikiwa na kuonekana kuwa hawakukidhi vigezo kwenye 
programu walizochaguliwa kuweza kuomba programu wanazokidhi vigezo 
kwenye dirisha hili; na wale ambao taarifa zao hazikukamilika, vyuo vitumie 
nafasi hiyo kurekebisha taarifa hizo.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA