MAJINA 28,202 ya Walioitwa kwenye Usaili Mwalimu Daraja La Iii C Kiswahili

MAJINA 28,202 ya Walioitwa kwenye Usaili Mwalimu Daraja La Iii C Kiswahili
MAJINA 28,202 ya Walioitwa kwenye Usaili Mwalimu Daraja La Iii C Kiswahili

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya MDAs & LGAs anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 29/10/2024 hadi 16/11/2024 hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  • Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Barakoa (Mask)
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura,Kitambulisho cha kazi,Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au barua ya utambulisho kutoka Serikali ya Mtaa/Kijiji unachotoka.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa,kidato cha IV, VI, Astashahada, Stashahada,Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hatiza matokeo za kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali alipopangiwa kufanyia usaili..Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA)
  • Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa iku ya usaili.

Post a Comment

Previous Post Next Post

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA