MAELEZO ya Kujiunga na Chuo Cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College) 2025

MAELEZO ya Kujiunga na Chuo Cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College) 2025
MAELEZO ya Kujiunga na Chuo Cha Ufundi Arusha (Arusha Technical College) 2025

MAELEZO YA KUJIUNGA NA MASOMO YA UFUNDI (VETA) KWA MWAKA WA MASOMO 2024/2025

Chuo kinatoa mafunzo kwa wale wanaotaka kufanya mitihani ya taifa ya Ufundi na kupata cheti cha ufundi 
yaani National Vocational Awards katika hatua NVA level 1

ORODHA YA KOZI (FANI) ZINAZOTOLEWA ZENYE NAFASI
Waombaji wanayo nafasi ya kujiendeleza katika mojawapo ya kozi (fani) zifuatazo:

A. KAMPASI (CAMPUS) YA ARUSHA MJINI (MAIN CAMPUS)
  • Biashara (Business Operation Assistant)
  • Utalii (Tour Guiding)
  • Ukataji na Uchongaji wa Madini (Gemstone Cutting and Polishing)
  • Uchoraji wa Ramani (Civil Draughting)
  • Maabara Msaidizi (Laboratory Assistant)
  • Tehama (Information and Communication Technology)
  • Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics)
  • Ufundi wa Umeme wa Magari (Auto Electrical)
  • Ufundi wa Umeme wa Majumbani (Domestic Electrical Installation)
  • Ufundi Electroniki (Electronics)
  • Ufundi Ujenzi (Masonry and Brick Laying)
  • Ujenzi na ukarabati wa barabara (Road Construction and Maintenance)
  • Ufundi Selemara (Carpentry and Joinery)
  • Ufundi wa Viyoyozi na Majokofu (Refrigeration and Air Conditioning)
  • Ufundi Mitambo (Fitter Mechanics)
  • Ufundi wa Uchomeleaji na Uhunzi wa Vyuma (Welding and Metal Fabrication)
  • Ufundi Bomba (Plumbing and Pipe Fitting)
  • Ufundi wa Uchongaji wa Vyuma na Vipuli (Fitting and Machining)
B. KAMPASI (CAMPUS) YA KIKULETWA
  • Ufundi Bomba (Plumbing and Pipe Fitting)
  • Ufundi Ujenzi (Masonry and Brick Laying)
  • Ufundi wa Umeme wa Majumbani (Domestic Electrical Installation)
  • Ufundi wa Mitambo ya Uzalishaji wa Umeme wa Maji (Hydropower Plants Maintenance)
  • Ufundi wa Umeme wa Mfumo wa Jua (Solar Energy)
  • Ufundi wa Umeme wa Mfumo wa Nishati Taka (Bio-Energy)
  • Ufundi wa Umeme wa Mfumo wa Upepo (Wind Energy)
SIFA ZA KUJIUNGA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (Arusha Technical College) 2024/2025
  • Mwombaji awe amemaliza kidato cha nne (Form Four) na kupata cheti cha kidato cha nne (Certificate of Secondary Education Examination - CSEE) cha Baraza la Mitihani la Taifa.
MAELEKEZO KWA WAOMBAJI
  • Kila mwombaji anatakiwa kuchagua “kozi/fani” moja tu kwa mwaka.
  • Masomo yatafundishwa kuanzia saa saba na nusu mchana (01:30PM) na kumalizika saa kumi na mbili na nusu jioni (06:30PM). Hivyo basi,
  • waombaji wote wanatakiwa wakati wa asubuhi wawe na sehemu ya kufanya mazoezi ya ufundi viwandani au katika karakana zinazohusiana na fani wanayoomba, ili waweze kuzingatia vizuri masomo watakayopata wakati wa jioni.
KUENDELEA NA ELIMU YA JUU
Wanafunzi watakaoendelea mpaka kufanikiwa kupata cheti cha mwaka wa tatu (NVA III) na kuwa na cheti 
cha kidato cha nne cha baraza la mitihani wataweza kupata nafasi ya kuendelea na chuo kwa masomo ya stashahada ya uhandisi (Diploma in Engineering) katika moja ya fani zifuatazo:
  • Stashahada ya Uhandisi Umeme (Diploma in Electrical Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi Ujenzi (Diploma in Civil Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi Umeme wa Maji (Diploma in Electrical and Hydropower Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi wa Mitambo ya Mafuta na Gesi (Diploma in Pipe Works, Oil and Gas  Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi Mitambo (Diploma in Mechanical Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi Mawasiliano (Diploma in Telecommunication Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi Usafirishaji (Diploma in Transportation Engineering)
  • Stashahada ya Sayansi na Teknolojia ya Maabara (Diploma in Laboratory Science)
  • Stashahada ya Tehama (Diploma in Information Technology/Diploma in Computer Science)
  • Stashahada ya Uhandisi Magari (Diploma in Automotive Engineering, Auto Electrical and Electronic Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi Umeme wa Jua (Diploma in Solar Energy Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi Umeme wa Upepo (Diploma in Wind Energy Engineering)
  • Stashahada ya Uhandisi Umeme wa Nishati Taka (Diploma in Bio-Energy Engineering)
MAMBO YA KUZINGATIA KWA WAOMBAJI
Kila mwombaji anapaswa kuzingatia mambo yafuatayo:
  • Gharama ya fomu ni shilingi Elfu Ishirini za Tanzania tu (20,000/=). Fedha hii ikishalipwa HAITARUDISHWA. (HATUPOKEI PESA TASLIMU). Wakati wa kufanya malipo ya fomu fika ofisi ya uhasibu Chuo cha Ufundi Arusha ili kupata Control Number. Au 
  • Fomu ya maombi irudishwe Ofisi ya Msajili kabla ya tarehe 20/12/2024 pamoja na (passport size) moja na ankara ya malipo ya ada (Pay in- slip)
  • Angalizo: Ada ikishalipwa haitarudishwa kwa sababu yoyote ile.
  • Fomu zitakazorudishwa baada ya tarehe hiyo hazitapokelewa.
  • Usaili (interview) itafanyika tarehe 06/01/2025 SAA MOJA KAMILI ASUBUHI.
  • Usajili utafanyika 13/1/2025 hadi 24/1/2025
  • Masomo yataanza rasmi Jumatatu tarehe 20/01/2025.
  • Mwombaji ahakikishe majina yaliyotumika katika cheti cha kidato cha nne (Form Four Certificate) ndiyo yatumike kujaza fomu hii ya maombi.
Soma maelekezo zaidi kwenye PDF hapa chini:
BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD PDF YA MAELEZO YA KUJIUNGA NA MASOMO YA UFUNDI (VETA) KWA MWAKA WA MASOMO 2024/2025
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA