M-koba ni huduma ya kuchanga Kidijitali yenye lengo mahususi la kuviwezesha vikundi mbalimbali vya kutunza fedha kama Vikundi vya Kifamilia/Marafiki, VICOBA, VSLA na SACOSS kuweza kuchanga fedha, kutunza fedha, kupeana mikopo, riba na kufanya mambo mengine kwa usalama, urahisi na akiwa popote.
Piga *150*00# > chagua Huduma za Kifedha > Chagua M-Koba.
Katika jitihada za kurahisisha shughuli za vikundi vidogo vya kutunza akiba, Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na Benki ya TPB wamezindua huduma ya kwanza na ya kipekee nchini kwaajili ya vikundi vya kuweka akiba vilivyo rasmi (VICOBA) na visivyo rasmi iitwayo M-Koba.
Huduma hii mpya ya M-Pesa itawezesha vikundi kutunza fedha kidijitali, kwa usalama na uwazi zaidi.
Suluhisho hili linalenga kusaidia mahitaji ya vikundi rasmi vya kuweka akiba na mikopo (VICOBA, VSLAs, CB) pamoja na vikundi mbali mbali visivyo rasmi.
Inakadiriwa kuwa asilimia 16 ya watanzania (zaidi ya watu milioni 4.4), wengi wao wakiwa wanawake, ni wanachama wa vikundi zaidi ya 50,000 vya kuweka akiba na mikopo (VICOBA) ambao huhifadhi akiba zaidi ya TZS bilioni 100 kwa mwaka.
Mbali na vikundi hivyo rasmi, kuna idadi ya zaidi ya vikundi 50,000 visivyo rasmi ambavyo vinaweka akiba na kutoa mikopo kupitia mitandao ya vikundi vya wahitimu, vyama vya kifamilia, vikundi vya watu wanaofanya kazi sehemu moja na kadhalika.
Huduma hii itaongeza angalau moja ya tatu ya idadi ya watu waliosajiliwa katika mifumo rasmi ya kifedha, na zaidi kufikia wanawake wa vijijini, ambao ndio asilimia kubwa zaidi ya idadi hiyo.
Kwa kuimarisha shughuli za vikundi vya akiba kidijitali zaidi, huduma hii itatengeneza mazingira wezeshi ambayo yatakuza utamaduni wa kuweka akiba, usimamizi imara wa kifedha na kukuza ujumuishwaji wa fedha nchini kwa njia ya M-Pesa.
AINA YA VIKUNDI KWENYE M-KOBA
Familia/Marafiki
- Hii ni akaunti maususi kwa vikundi vidogo inaweza kuwa familia ama marafiki ambao wamekusudia kuchanga fedha na baadae kugawana baada ya muda Fulani.
- Hii ni akaunti maususi kwa ajili ya vikundi vyenye upana mkubwa wa wanachama na vilivyo na mfumo wa kuuza na kununua hisa, kuweka akiba, Michango ya Kijamii na Kupeana Mikopo. Vikundi hivi ni vile vihusishavyo VICOBA/VSLA/CB/SILC.
- M-Koba imeletwa ili kutatua changamoto mbalimbali ambazo vikundi vinakutana nazo katika mfumo wa kutumia pesa taslimkama usalama mdogo wa fedha zinazokusanywa, wanavikundi kutokuwa urahisi wa kukusanya pesa.
Inaleta Usalama wa fedha za wanakikundi
- Mwanakikundi kuweza kuchangia kupitia simu yake popote alipo na kufikisha mchango wake kwa usalama na kwa wakati muda wowote.
- Endapo pesa itaingia au kutoka kwenye kikundi wajumbe na viongozi wote watapokea Ujumbe mfupi kuwajulisha.
Urahisi na Unafuu kwa Wana kikundi
Hakuna makato yoyote kutoa hela M-Pesa kwenda Kwenye akaunti ya kikundi au kutoa hela kutoka kwenye Akaunti ya kikundi kwenda kwenye akaunti ya M-Pesa ya mwanachama.
Mitandao Mingine
- Wanachama wa mitandao yote huweza kujiunga na Kikundi.