M-Koba Mfumo mpya wa VICOBA - PDF Jinsi ya kufungua Akaunti ya M-KOBA

M-Koba Mfumo mpya wa VICOBA - PDF Jinsi ya kufungua Akaunti ya M-KOBA
M-Koba Mfumo mpya wa VICOBA - PDF Jinsi ya kufungua Akaunti ya M-KOBA, JINSI ya Kujiunga na M-koba Vodacom, Jinsi ya Kuchangia M-koba,Tanzania Commercial Bank - PDF Jinsi ya kufungua Akaunti ya M-KOBA.

M-koba ni huduma ya kuchanga Kidijitali yenye lengo mahususi la kuviwezesha vikundi mbalimbali vya kutunza fedha kama Vikundi vya Kifamilia/Marafiki, VICOBA, VSLA na SACOSS kuweza kuchanga fedha, kutunza fedha, kupeana mikopo, riba na kufanya mambo mengine kwa usalama, urahisi na akiwa popote.

Piga *150*00# > chagua Huduma za Kifedha > Chagua M-Koba.

Katika jitihada za kurahisisha shughuli za vikundi vidogo vya kutunza akiba, Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na Benki ya TPB wamezindua huduma ya kwanza na ya kipekee nchini kwaajili ya vikundi vya kuweka akiba vilivyo rasmi (VICOBA) na visivyo rasmi iitwayo M-Koba.

Huduma hii mpya ya M-Pesa itawezesha vikundi kutunza fedha kidijitali, kwa usalama na uwazi zaidi.

Suluhisho hili linalenga kusaidia mahitaji ya vikundi rasmi vya kuweka akiba na mikopo (VICOBA, VSLAs, CB) pamoja na vikundi mbali mbali visivyo rasmi.

Inakadiriwa kuwa asilimia 16 ya watanzania (zaidi ya watu milioni 4.4), wengi wao wakiwa wanawake, ni wanachama wa vikundi zaidi ya 50,000 vya kuweka akiba na mikopo (VICOBA) ambao huhifadhi akiba zaidi ya TZS bilioni 100 kwa mwaka.

Mbali na vikundi hivyo rasmi, kuna idadi ya zaidi ya vikundi 50,000 visivyo rasmi ambavyo vinaweka akiba na kutoa mikopo kupitia mitandao ya vikundi vya wahitimu, vyama vya kifamilia, vikundi vya watu wanaofanya kazi sehemu moja na kadhalika.

Huduma hii itaongeza angalau moja ya tatu ya idadi ya watu waliosajiliwa katika mifumo rasmi ya kifedha, na zaidi kufikia wanawake wa vijijini, ambao ndio asilimia kubwa zaidi ya idadi hiyo. 

Kwa kuimarisha shughuli za vikundi vya akiba kidijitali zaidi, huduma hii itatengeneza mazingira wezeshi ambayo yatakuza utamaduni wa kuweka akiba, usimamizi imara wa kifedha na kukuza ujumuishwaji wa fedha nchini kwa njia ya M-Pesa.

M-Koba Mfumo mpya wa VICOBA - PDF Jinsi ya kufungua Akaunti ya M-KOBA
AINA YA VIKUNDI KWENYE M-KOBA

Familia/Marafiki

  • Hii ni akaunti maususi kwa vikundi vidogo inaweza kuwa familia ama marafiki ambao wamekusudia kuchanga fedha na baadae kugawana baada ya muda Fulani.
VICOBA/VSLA/SACCOS
  • Hii ni akaunti maususi kwa ajili ya vikundi vyenye upana mkubwa wa wanachama na vilivyo na mfumo wa kuuza na kununua hisa, kuweka akiba, Michango ya Kijamii na Kupeana Mikopo. Vikundi hivi ni vile vihusishavyo VICOBA/VSLA/CB/SILC.
Faida za Kutumia M-Koba:

  • M-Koba imeletwa ili kutatua changamoto mbalimbali ambazo vikundi vinakutana nazo katika mfumo wa kutumia pesa taslimkama usalama mdogo wa fedha zinazokusanywa, wanavikundi kutokuwa urahisi wa kukusanya pesa.
Hivyo M-Koba huleta:

Inaleta Usalama wa fedha za wanakikundi

  • Mwanakikundi kuweza kuchangia kupitia simu yake popote alipo na kufikisha mchango wake kwa usalama na kwa wakati muda wowote.

Uwazi kwa Wanakikundi/Wanachama

  • Endapo pesa itaingia au kutoka kwenye kikundi wajumbe na viongozi wote watapokea Ujumbe mfupi kuwajulisha.

Urahisi na Unafuu kwa Wana kikundi

Hakuna makato yoyote kutoa hela M-Pesa kwenda Kwenye akaunti ya kikundi au kutoa hela kutoka kwenye Akaunti ya kikundi kwenda kwenye akaunti ya M-Pesa ya mwanachama.

Mitandao Mingine

  • Wanachama wa mitandao yote huweza kujiunga na Kikundi.

Jinsi ya kufungua Akaunti ya M-KOBA, Kuchangia, Kuongeza Mwanachama, Kuchangia Kutoka Mitandao Mingine na Maelekezo mengine ya Utumiaji wa Kikundi Cha M-koba tafadhali download PDF iliyoambatanishwa hapa chini; 
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA