JINSI ya Kujiunga na Songesha - Ada ya Songesha Vodacom

JINSI ya Kujiunga na Songesha - Ada ya Songesha Vodacom
JINSI ya Kujiunga na Songesha - Ada ya Songesha Vodacom

Vodacom kwa kushirikiana na TPB Bank katika kutambua mahitaji ya wateja wake imewaletea huduma mpya na ya kipekee kabisa ambayo kazi yake ni kukusaidia pale salio lako la M-Pesa linapokuwa halitoshi kukuwezesha kukamilisha miamala yako ya M-Pesa.

Huduma hii inaitwa Songesha. Songesha ni huduma inayokuwezesha kumalizia miamala yako bila kukwama endapo salio lako la M-Pesa ni pungufu.

Ukiwa na Songesha utaweza kukamilisha miamala ya kutuma pesa, kulipia huduma na bidhaa kwa makampuni pamoja na kukamilisha miamala ya kulipa kwa M-Pesa kwa wafanyabiashara wanaopokea malipo kwa M-Pesa kutoka kila kona ya Tanzania.

Hata ukiwa na salio pungufu la M-Pesa, malizia miamala bila kwikwiNi rahisi.

Piga *150*00# chagua Huduma za kifedha kisha.

JINSI ya Kujiunga na Songesha - Ada ya Songesha Vodacom
MAELEKEZO JINSI YA KUJIUNGA NA SONGESHA, KUTUMIA NA ADA ZAKE DONWLOAD PDF HAPA.

 Je ni vigezo vipi natakiwa kutimiza ili kutumia huduma ya SONGESHA?

  • Ili kutumia huduma ya SONGESHA inabidi uwe unatumia M-Pesa na mtandao wa Vodacom. Hivyo utatakiwa kujiunga kwa kuingia kwenye Menyu ya M-Pesa kisha kukubali vigezo na masharti.

Je ni akaunti ngapi naweza kutumia kujiunga na SONGESHA?

  • Kila laini ya Vodacom iliyosajiliwa na M-Pesa kwa angalau miezi mitatu ina uwezo wa kutumia SONGESHA. Kama wewe ni mteja mpya wa Vodacom tumia huduma za M-Pesa kwa angalau miezi mitatu uanze kunufaika na huduma hii.

Je kiwango cha Matumizi ni nini?

  • Hiki ni kiwango cha juu ambacho utaweza kutumia kwenye huduma ya SONGESHA kwa mwezi. Kiwango hiki kitapanda au kushuka kulingana na matumizi yako. Mwenendo mzuri wa marejesho na matumizi ya M-Pesa na SONGESHA utapelekea kuongezeka kwa kiwango cha Songesha. Mwenendo mbaya utasababisha kushuka kwa kiwango au kukusababishia kufungiwa huduma ya SONGESHA. 

Je ni miamala gani inaweza kukamilishwa kupitia SONGESHA?

  • SONGESHA itakuwezesha kukamilisha miamala ifuatayo tu: Kutuma pesa kwa wateja wa M-Pesa walio sajiliwa.Kulipia BILI kama LUKU, Malipo ya Serikali, Huduma za Usafiri, Malipo ya Ving’amuzi n.k.Kulipa kwa wafanyabiashara walio sajiliwa na huduma ya Lipa kwa M-Pesa.

Je nitaweza kutumia SONGESHA mara ngapi?

  • Utaweza kutumia huduma ya SONGESHA kukamilisha Miamala mitano kwa nyakati tofauti mpaka utakapolipa ndipo utakapoweza kutumia huduma nyingine ya SONGESHA.

Je nitawezaje kutumia kiwango changu cha SONGESHA?

  • Utatakiwa kufanya miamala ya M-Pesa kama kawaida na pale unapokuwa hauna salio la kutosha la kukamilisha miamala iliyoruhusiwa SONGESHA itatumika kukamilisha muamala huo.

Je kuna gharama/makato yoyote ya kutumia huduma ya SONGESHA?

  • Unapotumia huduma ya SONGESHA utalipa gharama ya Ada ya Maombi kulingana na kiwango unachopewa. Ada hii itatozwa mara moja tu pale utakapotumia huduma ya SONGESHA. Pia utatozwa ada ya huduma kwa siku ambayo ni 1% ya kiwango ulichopewa.
Ada ya Songesha Vodacom

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA