Yanga imemrejesha Edna Lema ambaye alikaribia kuipa Yanga Princess Ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake 2022/2023.
Uongozi wa Yanga umefikia maamuzi hayo ya kumrejesha Edna Lema katika Kikosi Cha Yanga Princess baada ya misimu miwili isiyoridhisha.
Jukumu la kwanza la Lema litakuwa kukisuka upya kikosi cha Yanga Princess ambapo ni kama kazi imeanza upya baada ya kuachana na idadi kubwa ya wachezaji waliotumika msimu uliopita
Lema ana uzoefu mkubwa na soka la Wanawake ambapo alicheza kwa mafanikio kabla ya kuchukua majukumu ya ukufunzi.