VIONGOZI Chama cha Soka Mkoani Mwanza Lawamani

VIONGOZI Chama cha Soka Mkoani Mwanza Lawamani
VIONGOZI Chama cha Soka Mkoani Mwanza Lawamani

WADAU wa Soka Mkoani Mwanza wamesema kuwa mgogoro wa Soka uliopo katika mkoa wa Mwanza unasababisha na uongozi wa Chama cha Soka kwa kutokufuata Katiba ya Chama hicho.

Wakizungumza mbele ya waandishi wa Habari katika Ukumbi wa Lake Hotel Mwanza, wadau hao wamesema kuwa pamoja na jitihada zinazofanywa na chama cha soka, Viongozi wake wamefeli sehemu kubwa katika kuleta maendeleo ukilinganisha na mikoa mingine.

Mmoja wa Wadau hao, Munga Lupindo ambaye amewahi kuwa  Mwenyekiti wa Soka wa Wilaya ya Nyamagana amesema kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho (MZFA), Vedasto Lufano amekosa sifa na uhalali wa kuendelea kuongoza chama hicho.

"Toka wachaguliwe mwaka 2020 hadi leo hawajaitisha Mkutano mkuu wa Wanachama ili kuzungumzia maendeleo ya Soka la Mwanza. Pamoja na hilo kusoma mapato na matumizi ya kila Mwaka, halijawahi kufanyika" alisema Munga Lupindo.

"Mwenyekiti wa MZFA, Vedasto Lufano amekuwa kama Mungu, anadharau kila mtu hapa mkoani, na sio kudharau tu mpaka matusi anawatukana. Ukimshauri au kuwa kinyume na yeye kwenye mawazo, anakuchukia kabisa" 

"Hatuwezi kuwa na chama cha mtu, hiki ni chama cha wanachama, kwanini mtu mmoja anataka aogopwe? Mfano mimi sikumuunga mkono kwenye uchaguzi uliopita mpaka leo ni adui kwake".

VIONGOZI Chama cha Soka Mkoani Mwanza Lawamani
Naye Kessy Mziray ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Makocha mkoani Mwanza (TAFCA) amesema kuwa anashangaa chama hicho kinavyoendeshwa. Yeye alikuwa mjumbe wa kamati tendaji kwa mujibu wa Katiba ila aliondolewa kinyemela na Mwenyekiti bila kufuata utaratibu.

"Hata kabla ya mabadiliko ya Katiba mpya, mimi nilikuwa sipewi taarifa za kikao, na hata pale nilipokuwa nimefahamu na kwenda kwenye kikao, Mwenyekiti alikuwa ananitoa nje bila sababu za msingi" 

"Mara kwa mara nilikua najitahidi kuuliza huenda tatizo langu liko wapi, na taarifa zinazopewa ni kwamba mimi sistahili kuwa kwenye kikao cha kamati tendaji maana inasemekana niko kinyume na Mwenyekiti wa MZFA"

"Kinachoshangaza ndugu waandishi wa Habari, Mwenyekiti wa MZFA ameufanya mpira wa Mwanza kama wa familia yake. hataki kuambiwa chochote wala ushauri wowote"

"Mfano kwa miaka yote hii minne Chama hakina Mtunza Hazina wake maana kipindi cha uchaguzi kura zake hazikutosha" na haukufanyika uchaguzi wa kujaza nafasi hiyo hadi leo. Katibu wa Chama ndio Katibu na huyo huyo ndio Mhasibu wakisaidiana na Mwenyekiti" alisema Kessy Mziray.

"Kwa hali hii hakuna uwazi wa mapato na matumizi ya chama kwa miaka yote minne wakiwa madarakani. Wajumbe wanaokuwa na uwezo wa kuhoji huwa wanaondolewa kwenye nafasi hiyo hasa wale wa kuteuliwa au wa kuingia kwa sababu Katiba imetamka hivyo"

Frank Masamaki Kamalamo mdau wa soka Mkoani Mwanza naye aliwashutumu viongozi wa Chama cha soka kwa kushindwa kuwajibika kwa wanaowaongoza. Wamekuwa wakifanya mambo kwa maslahi yao na sio maslahi ya Mkoa, na kuomba wajiuzulu.

"Tunaomba Kamati ya Maadili ya (TFF) kuwachunguza Viongozi hawa wa (MZFA), hawastahili kuwepo ofisini kwa sababu wamekiuka katiba. Sisi kama wadau tumechoshwa na uongozi wao" alisema Kamalamo.

"Unashangaa chaguzi za Vyama vya wilaya zimeanza kufanyika bila kutangazwa. Unasikia mara Misungwi, Magu na Sengerema wameshafanya uchaguzi bila kufuata taratibu na miongozo yake"

"Watu wanachaguliwa kinyemela ili waje kuwapigia kura kwenye uchaguzi wa Mkoa ili waendelee kukaa madarakani huku wakiendelea kuharibu soka letu la Mwanza"

"Pia tunamuomba Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mohamed Mtanda kufuatilia Masuala haya maana hayana afya katika mkoa wetu na kuyapatia ufumbuzi wa haraka maana tusipoziba ufa tutajenga ukuta" alisema Kamalamo.

Mwenyekiti wa MZFA, Vedasto Lufano alipopigiwa simu na Mwandishi wa Habari wa Clouds Mwanza kwa Niaba ya wengine kuzungumzia suala hakuwa tayari kuzungumza maana alipokea na kukaa kimya hadi simu ikakatika.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA