Klabu ya Simba Sports Club inatarajiwa kucheza mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF Confederation Cup 2024/2025) dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.
Mchezo huo utachezwa Jumapili ya tarehe 22 September 2024 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar Es Salaam kuanzia saa 10:00 jioni.
Kuelekea mchezo huo klabu ya Simba imetangaza viingilio ambapo mzunguuko itakuwa ni Tsh 3,000 huku viti vya rangi ya Machungwa ikiwa ni Tsh 5,000.