TCU Udahili wa Shahada ya Kwanza Awamu ya Pili 2024-2025

TCU Udahili wa Shahada ya Kwanza Awamu ya Pili 2024-2025

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) inaufahamisha umma, Taasisi za Elimu ya Juu na wadau wa Elimu ya Juu ndani na nje ya nchi kuwa Awamu ya Kwanza ya udahili wa Shahada ya Kwanza katika Taasisi za Elimu ya Juu nchini kwa mwaka wa masomo 2024/2025 imekamilika. 

Majina ya waliodahiliwa katika awamu hii yametangazwa na vyuo husika. 

Katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 124,286 wametuma maombi ya kujiunga katika vyuo 86 vilivyoidhinishwa kudahili wanafunzi katika Shahada ya Kwanza.

Aidha, jumla ya programu 856vzimeruhusiwa kudahili ikilinganishwa na programu 809 mwaka 2023/2024, ikiwa ni ongezeko la programu 47 za masomo.

Vilevile kwa upande wa nafasi za udahili, mwaka huu kuna jumla ya nafasi 198,986 ikilinganishwa na nafasi 186,289 mwaka uliopita. 

Hili ni ongezeko la nafasi 12,697 sawa na asilimia 6.8 katika programu za Shahada ya Kwanza.

Pia katika Awamu ya Kwanza ya udahili, jumla ya waombaji 98,890 sawa na asilimia 79.6 ya waombaji wote walioomba udahili, wamepata udahili kwenye vyuo walivyoomba.

Idadi ya waombaji wa udahili na watakaodahiliwa inatarajia kuongezeka katika Awamu ya Pili ya udahili.

WAOMBAJI WALIODAHILIWA KATIKA CHUO ZAIDI YA KIMOJA

Waombaji waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja wanapaswa kuthibitisha udahili wao katika chuo kimojawapo kuanzia tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2024.

Uthibitisho huo unafanyika kwa kutumia namba maalum ya siri iliyotumwa kwa ujumbe mfupi kupitia namba zao za simu au barua pepe walizotumia wakati wa kuomba udahili.

Wale ambao hawatapata kwa wakati ujumbe huo, wanashauriwa kuingia kwenye mifumo ya udahili ya vyuo walivyodahiliwa na kuomba kutumiwa ujumbe mfupi wenye namba maalum ya siri ili kuweza kujithibitisha katika chuo husika. 

Aidha, uthibitisho wa udahili ufanyike kupitia akaunti ambayo muombaji alitumia wakati wa kuomba udahili.

Kwa urahisi wa rejea, orodha ya majina ya waliodahiliwa katika chuo zaidi ya kimoja inapatikana kwenye tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz). 

KUFUNGULIWA KWA AWAMU YA PILI YA UDAHILI 2024/2025

Tume inatangaza kuwa Awamu ya Pili ya udahili wa Shahada ya Kwanza kwa mwaka wa masomo 2024/2025 imeanza leo tarehe 03 hadi 21 Septemba, 2024.

Tume inawaasa waombaji ambao hawakuweza kutuma maombi ya udahili au hawakuweza kupata nafasi ya kudahiliwa katika Awamu ya Kwanza kutokana na sababu mbalimbali, watumie fursa hii vizuri kwa kutuma maombi yao ya udahili kwenye vyuo wanavyovipenda. 

Aidha, Tume inaelekeza Vyuo vya Elimu ya Juu nchini kutangaza programu ambazo bado zina nafasi.

Waombaji udahili na vyuo wanapaswa kuzingatia utaratibu wa udahili wa Awamu ya Pili kama ilivyooneshwa kwenye kalenda ya udahili iliyoko katika tovuti ya TCU (www.tcu.go.tz).

WITO KWA WAOMBAJI UDAHILI

Waombaji udahili wa Shahada ya Kwanza wanakumbushwa kuwa masuala yote yanayohusu udahili au kujithibitisha katika chuo kimoja yawasilishwe moja kwa moja kwenye vyuo husika.

Kwa wale ambao watapata changamoto katika kujithibitisha, vyuo vyote vimeelekezwa kupokea taarifa zao na kutafuta ufumbuzi wa haraka kwa kuzingatia miongozo na taratibu zilizowekwa. 

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA