TAAARIFA MPYA KWA WASAILIWA WA KADA ZA AFYA

TAAARIFA MPYA KWA WASAILIWA WA KADA ZA AFYA

Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ilianzishwa kwa mujibu wa kifungu 29 (1) cha Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 iliyorejewa 2019, ambayo inaelekeza kuwepo kwa chombo maalumu cha kushughulikia mchakato wa Ajira katika Utumishi wa Umma.

Usaili wa Kada za Afya ulianza tarehe 02 Septemba, 2024 mpaka tarehe 13 Septemba, 2024, lengo likiwa ni kujaza nafasi wazi 9483, na wale watakaofaulu Usaili wa Mahojiano lakini hawakuweza kupangiwa vituo vya kazi (Kanuni ya 22 ya Kanuni za uendeshaji wa shughuli za Sekretarieti ya Ajira za 2021 zilizorekebishwa 2022, watabaki kwenye Kanzi data na kupangiwa vituo vya kazi kulingana na upatikanaji wa vibali.

Usaili wa Mahojiano unatarajiwa kuanza tarehe 09 Septemba, 2024 mpaka tarehe 13 Septemba, 2024.

Hivyo, wasailiwa wote wanatakiwa kwenda kwenye Usaili wa Mahojiano kulingana na jina la Mwajiri (Employer) linaloonekana katika Akaunti ya Msailiwa ya Ajira Portal.

Aidha, Wasailiwa wasisahau kubeba Vyeti Halisi - Cheti cha kuzaliwa, Cheti cha Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Vyeti vya taaluma, Leseni Hai ya Kutoa huduma na Kitambulisho Halisi kati ya kitambulisho cha Uraia (NIDA), Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga Kura, Hati ya Kusafiria, Leseni ya Udereva, Kitambulisho cha Kazi au Barua ya Utambulisho kutoka Ofisi ya Serikali ya Mtaa unaoishi/Shehia kwaajili ya Utambuzi.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA