SIMBA YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA , SANDALAND THE ONLY ATOA PUNGUZO LA JEZI

SIMBA YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA , SANDALAND THE ONLY ATOA PUNGUZO LA JEZI
SIMBA YAWAITA MASHABIKI KWA MKAPA , SANDALAND THE ONLY ATOA PUNGUZO LA JEZI

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba SC, Ahmed Ali amesema kuwa nguvu ya wanamsimbazi wote inahitajika siku ya Jumapili katika mchezo wa pili kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho barani Afrika 2024/2025.

Ahmed amewataka mashabiki hao kununua tiketi kwa wingi kuhakikisha wanaujaza uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo dhidi ya Al Ahli Tripoli ya Libya.

Ahmed ameongeza kuwa wachezaji wanahitaji sapoti ya mashabiki ili kuhakikisha wanashinda na kutinga hatua ya makundi, huku akisema kuwa yatakuwa makosa makubwa kwa mashabiki wa Simba kuamua kubaki nyumbani wakiamini Simba imemaliza kazi baada ya kupata suluhu ugenini.

"Lazima tutambue kwamba huu mchezo bado upo 50% kwa 50%. Atakayechanga vizuri karata zake ndio atakwenda makundi sababu mchezo wa kwanza ulikuwa sare lakini sisi tunayo faida. Kwao walishindwa kutumia faida ya kuwepo mashabiki zao uwanjani, sisi tutaitumia. Mtu asiregeze masikio kwamba tutafuzu kirahisi, mechi hii bado ni mbichi"

"Sisi tusimame na Simba yetu bila kuangalia ukubwa wa shindano. Kila Mwanasimba ajiulize mwenyewe kwanza kushindwa nyumbani kwetu, pili kushindwa kufuzu makundi ya Kombe la Shirikisho. Tuamke sasa kuipambania Simba yetu ili ifuzu makundi"

"Mechi ya kule Libya tuliachia benchi la ufundi na wachezaji wapambane. Mechi ya Septemba 22 ni mechi yetu wote Wanasimba, Jumapili twendeni uwanjani kushangilia timu yetu, tukaipeleke timu yetu makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika."

"Mpaka sasa tupo nyuma goli 2-0 dhidi ya mashabiki wa Al Ahli Tripoli. Goli la kwanza kuujaza uwanja wao wote kwa mashabiki 50,065. Hili kwetu ni deni na sisi kuujaza. Sina hofu na hilo kujaza uwanja wa Mkapa. Wao walijaa na sisi tunapaswa kujaa. Goli la pili mashabiki wote kuvaa jezi za timu yao, na hilo tuna wajibu wa kwenda kusawazisha. Kila Mwanasimba atakayekuja uwanjani anatakiwa kuvaa jezi mpya ya msimu hii," alisema Ahmed

Katika hatua nyingine, Sandaland The Only One wametoa ofa ya punguzo bei ya jezi kuelekea mchezo huo ambapo jezi zitauzwa Tsh 30,000/- katika maduka yote ya Sandaland.

"Kwa kutambua kwamba tunapaswa kuvaa jezi za aina moja, mdhamini wetu wa jezi amepunguza bei kwa punguzo maalumu. Jezi zitauzwa Tsh. 30,000 na zinapatikana kwenye maduka ya Sandaland The Only One lakini pia kwa atakayekuja uwanjani na kununua jezi yake ya Tsh. 30,000 atampa zawadi ya tiketi ya mchezo bure"

Hamasa kuanzia Kibaha ambapo pia tawi jipya litazinduliwa.

“Kesho tutakwenda kufanya hamasa kule Kibaha na itaambatana na kufanya uzinduzi wa tawi. Wilaya ya Kibaha kuna Wanasimba wengi kwelikweli. Uzinduzi utaanza saa 4 asubuhi na msafara wa magari yasiyopungua 50 tutaondoka Magomeni saa 3 asubuhi.”

“Kibaha tutakuwa pia na gari maalumu la Sandaland The Only One kuuza jezi kwa punguzo la Tsh. 30,000 na tiketi zitauzwa hapo hapo. Wanasimba wote wanakaribishwa muhimu kuzingatia muda.”

“Ijumaa tutakuwa Mbagala kuwauzia Wanasimba tiketi, baada ya hapo tutaenda kula biryani na watoto yatima katika Hiyari Orphanage Centre kilichopo Mbagala Kizuiani. Wanasimba wote mnakaribishwa, wewe njoo na njaa yako.”

“Waamuzi wote wa mchezo wanatokea Guinea na match commissioner anatokea Somalia. Hawa ndio watasimamia mchezo.”

“Wote tuliona vurugu zilizotokea kwa mashabiki wao kwenye mchezo uliopita, ile ndio hurka yao. Na vurugu ziligusa makundi matatu, sisi, marefa na timu yao kwa kushindwa kutufunga. Walifanya vile kwa kujua kwamba shughuli yao iliishia pale, hawataweza kupata matokeo kwenye uwanja wetu wa nyumbani. Wanajua kwamba Dar es Salaam sio sehemu salama kwao na sisi tutawaonyesha kwa vitendo kwamba hawatoki salama.”- Ahmed Ally.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA