SIMBA YAITISHA MKUTANO MKUU WA KAWAIDA WA MWAKA 2024

SIMBA YAITISHA MKUTANO MKUU WA KAWAIDA WA MWAKA 2024
SIMBA YAITISHA MKUTANO MKUU WA KAWAIDA WA MWAKA 2024


Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Company Limited kwa mujibu wa Ibara 21(1) ya Katiba ya Simba Sports Club, 2018 (na marekebisho ya Januari, 2024) inawataarifu wanachama wake kuwa Mkutano mkuu wa kawaida wa mwaka 2024 utafanyika Oktoba 6, 2024 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Mkutano unatarajiwa kuanza saa 2 Asubuhi.

Agenda za mkutano huo ni kwa mujibu wa Ibara ya 22 ya katiba na zitawasilishwa sambamba na nyaraka kwa wanachama kupitia matawi yao kwa mujibu wa katiba.

Wanachama wote hai wanaalikwa kuhudhuria mkutano huo.

Post a Comment

Previous Post Next Post

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA