SIFA ZA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) 2024

SIFA ZA KUJIUNGA NA JESHI LA KUJENGA TAIFA (JKT) 2024
Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Nduku Mabele, anawataarifu Vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea kwa mwaka 2024.

Utaratibu wa Vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo, unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi.

Usaili wa Vijana hao kujiunga na Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa kujitolea utaanza tarehe 01 Oktoba, 2024 kwa Mikoa yote Tanzania bara na Visiwani.

Vijana watakaoteuliwa watatakiwa kuripoti kwenye Makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa kuanzia tarehe 01 Novemba, 2024 hadi 03 Novemba, 2024.

Sifa za kujiunga na JKT kwa
Kujitolea na Vifaa vinavyohitajika
  • Awe raia wa Tanzania.
  • Umri.
  • a.Kwa Vijana wenye Elimu ya Darasa la Saba umri ni kuanzia miaka 16 hadi 18, waliomaliza Elimu ya Msingi kuanzia Mwaka 2021, 2022, 2023 na awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Msingi
  • b.Vijana wenye Elimu ya Kidato cha Nne umri usiwe zaidi ya miaka 20, waliomaliza Elimu ya Sekondari kuanzia Mwaka 2021, 2022, 2023 na awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Sekondari (Secondary Leaving Certificate) na cheti halisi cha matokeo (Academic Certificate). Awe na ufaulu wa Daraja la Kwanza hadi Daraja la Nne. Kijana mwenye Daraja la Nne awe na ufaulu wa alama kuanzia 26 hadi 32.
  • C. Vijana wenye Elimu ya Kidato cha Sita umri usiwe zaidi ya miaka 22, waliomaliza Elimu ya Sekondari kuanzia Mwaka 2021, 2022, 2023 na awe na cheti halisi cha kumaliza Elimu ya Sekondari (Secondary Leaving Certificate) na cheti halisi cha matokeo (Academic Certificate). Awe na ufaulu wa Kuanzia Daraja la Kwanza hadi Daraja la Nne.
  • d. Vijana wenye Elimu ya Stashahada umri usiwe zaidi ya miaka 25, awe na vyeti vya Sekondari na cheti cha Chuo.
  • e. Vijana wenye Elimu ya Shahada umri usiwe zaidi ya miaka 26, awe na vyeti vya Sekondari na cheti cha Chuo.
  • f. Vijana wenye Elimu ya Shahada ya Uzamili umri usiwe zaidi ya miaka 27, awe na vyeti vya Sekondari na cheti cha Chuo.
  • Awe na Afya njema, Akili timamu na asiwe na alama yoyote ya michoro mwilini (Tattoo).
  • Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia Mahakamani na hajawahi kufungwa.
  • Awe na Kitambulisho cha Taifa au namba ya utambulisho Kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
  • Awe na cheti halisi cha kuzaliwa (Original Birth Certificate).
  • Asiwe ametumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo wala kuajiriwa na idara nyingine Serikalini.
  • Asiwe amepitia JKT Operesheni za nyuma kwa Kundi la kujitolea na Kundi la lazima (Mujibu wa Sheria).
  • Asiwe amejihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya, bangi na yanayofanana na hayo.
  • Angalizo: Kijana atakayepatikana na nyaraka za kughushi atachukuliwa hatua kali za kisheria kulingana na taratibu zilizopo.
Vifaa wanavyotakiwa kwenda navyo JKT
  • Bukta ya rangi 'Dark Blue' yenye mpira kiunoni (elastic) iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu, kwa vijana wa kike iwe na mpira kiunoni na kwenye pindo za miguu.
  • Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  • Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  • Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  • Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  • Truck suit ya rangi ya kijani au blue.
  • Fulana ya kijani kibichi yenye kola ya duara isiyo na maandishi.
  • Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA