RATIBA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024

RATIBA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024

RATIBA YA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara 145 na 146 inaelezea uwepo wa Serikali za Mitaa pamoja na madhumuni yake.

Mojawapo ya madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi.Aidha, Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288, zinaelekeza kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Lengo ni kuzifanya Serikali za Mitaa ziongozwe kidemokrasia.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 201A cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za
Wilaya) Sura 287 na Kifungu cha 87A cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka
za Miji) Sura 288, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ana mamlaka ya kutunga Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambazo hutumika kuongoza uchaguzi huo.

Viongozi wanaochaguliwa katika ngazi hizi ni wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, wenyeviti wa mitaa, wajumbe wa kamati za mitaa na wenyeviti wa vitongoji Uchaguzi wa mwisho wa Serikali za Mitaa ulifanyika mwezi Novemba mwaka 2019, hivyo, uchaguzi mwingine unatakiwa kufanyika Novemba, 2024.

Uchaguzi huu unaongozwa na Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya vijiji, Vitongoji na mitaa katika Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji, Matangazo ya Serikali Na. 571, 572 573 na 574 ya Mwaka 2024.

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, ninapaswa kutoa Tangazo la Uchaguzi likiainisha ratiba, shughuli za uchaguzi zinazohusika na masharti muhimu ya uchaguzi.

MASHARTI MUHIMU YA UCHAGUZI
Masharti muhimu ya kuzingatia katika Uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:-

(a) Nafasi zitakazogombewa:

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huu
ni:-

  • Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi
    mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka
    za Wilaya.Kwa nafasi hizo,uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa
    Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri
    ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 571 la Mwaka 2024),
  • Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo. Kwa nafasi hiyo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi
    wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo za Mwaka
    2024 (Tangazo la Serikali Na. 572 la Mwaka 2024)
  • Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi
    mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka za Miji. Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa
    Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za
    Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na.573 la Mwaka 2024) na
  • Mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji. Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa
    Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka
    za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 574 la Mwaka 2024).

(b) Majina na mipaka ya Vijiji na Vitongoji:

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, ili kuwafahamisha wananchi majina ya maeneo na mipaka ambayo itahusika katika kujiandikisha na upigaji wa kura,
wasimamizi wa uchaguzi watatangaza majina na mipaka ya vitongoji vilivyoko katika eneo la Halmashauri husika siku sabini na mbili kabla ya siku ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa mwenyekiti wa kitongoji, mwenyekiti wa kijiji, mwenyekiti wa mtaa, wajumbe wa Serikali ya Kijiji na wajumbe wa Kamati ya Mtaa.

(c) Maelekezo Kuhusu Uchaguzi:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Msimamizi wa uchaguzi atatoa maelekezo ya
Uchaguzi siku sitini na mbili kabla ya siku ya uchaguzi.

(d) Uteuzi wa Waandikishaji na Waandaaji wa Orodha ya Wapiga Kura:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Msimamizi wa Uchaguzi atafanya uteuzi wa watumishi wa umma watakaoandikisha na kuandaa Orodha ya Wapiga
Kura siku hamsini na mbili kabla ya siku ya Uchaguzi.

(e) Uandikishaji wa Wapiga Kura:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, uandikishaji na uandaaji wa Orodha ya wapiga kura utaanza siku ya arobaini na saba kabla ya siku ya uchaguzi na
utafanyika kwa muda wa siku kumi kwa kutumia fomu iliyoainishwa katika
Jedwali la Kwanza la Kanuni hizi katika majengo ya umma na pale ambapo hakuna jengo la umma, uandikishaji utafanyika kwenye sehemu ambayo Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atakuwa amekubaliana na viongozi wa vyama vya siasa.

(f) Vituo vya Kujiandikisha, Kupiga Kura na Kupigia Kura:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, vituo vya kujiandikisha kupiga kura na kupigia
kura, kwa maeneo yaliyo chini ya Halmashauri za Wilaya na Mamlaka za
Miji Midogo vitakuwa katika ngazi ya kitongoji. Kwa upande wa Mamlaka za
Miji (Miji, Manispaa na Majiji), vituo vya kujiandikisha kupiga kura na kupigia
kura vitakuwa katika ngazi ya mtaa.

(g) Muda wa Kuchukua na Kurudisha Fomu za Uteuzi:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Mtu yeyote anayekusudia kugombea nafasi za
uongozi, atatakiwa kuchukua fomu ya uteuzi wa kugombea nafasi husika
siku zisizopungua ishirini na sita kabla ya siku ya uchaguzi kwa kadri itakavyoelekezwa na Msimamizi wa Uchaguzi na kutakiwa kurejesha
fomu husika ndani ya muda wa siku saba tangu siku ya kwanza ya uchukuaji wa fomu iliyotangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi.

(h) Wagombea wa nafasi za Uongozi:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi
watatakiwa kuwa wanachama na wadhamininiwa wa Vyama vya Siasa
vyenye Usajili wa Kudumu.

(i)Utaratibu wa uteuzi wa wagombea:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atafanya uteuzi wa wagombea wa nafasi husika siku kumi na tisa kabla ya tarehe ya Uchaguzi kuanzia saa mbili kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.

(j) Utaratibu wa uteuzi wa mgombea pekee:
Endapo kutakuwa na mgombea mmoja halali wa nafasi ya uenyekiti wa
kijiji, kitongoji, ujumbe wa Halmashauri ya kijiji, uenyekiti wa mtaa au
ujumbe wa kamati ya mtaa Msimamizi Msaidizi wa uchaguzi atamteua mwombaji huyo kuwa mgombea pekee kwa nafasi aliyoomba.

(k) Pingamizi kuhusu uteuzi:
Mgombea au mtu aliyeomba kuteuliwa anaweza kuweka pingamizi kuhusu uteuzi wa wagombea. Pingamizi dhidi ya uteuzi wa wagombea litawasilishwa kwa maandishi kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika muda wa siku mbili tangu uamuzi au uteuzi ulipofanyika na
Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi atasikiliza na kutoa uamuzi katika
muda usiozidi siku mbili kuanzia siku ya kupokea pingamizi hilo.

(l) Kamati ya Rufani:
Kutakuwa na Kamati ya Rufani katika kila Wilaya ambayo itasikiliza pingamizi
kuhusu uteuzi wa wagombea katika Wilaya husika. Wajumbe wa Kamati ya
Rufani watateuliwa siku saba kabla ya siku ya uteuzi wa wagombea.

(m) Ukomo wa kuwa Madarakani:
Nafasi zote zinazogombewa zilikuwa na uongozi kwa kipindi cha miaka
mitano. Kwa mujibu wa Kanuni hizi, viongozi hao watakoma kushika
nafasi za uongozi siku saba kabla ya siku ya kuchukua fomu za kugombea uongozi chini ya Kanuni hizi.

(n) Upigaji wa Kura:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, kura zitapigwa katika namna itakayozingatia
usiri na kwa kutumia karatasi maalum za kupigia kura ambazo zitatakiwa
kutumbukizwa katika masanduku maalum ya kupigia kura.

(o) Waangalizi wa ndani wa uchaguzi:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Waangalizi wa Ndani wa Uchaguzi wataruhusiwa kuangalia uchaguzi baada ya kupata kibali cha Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa. Maombi ya kibali cha uangalizi wa uchaguzi yatawasilishwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa ndani ya muda wa siku ishirini na moja baada ya Tangazo la Uchaguzi kutolewa.

(p) Elimu ya Mpiga Kura:
kwa mujibu wa Kanuni hizi, taasisi yoyote inayotaka kutoa elimu ya mpiga
kura katika uchaguzi, itatakiwa kuwasilisha maombi ya kibali cha kutoa
elimu ya mpiga kura kwa Katibu Mkuu wa Wizara yenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Mwongozo wa Elimu ya Mpiga kura ulioandaliwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI.

(q) Kampeni za Uchaguzi:
Kwa mujibu wa Kanuni hizi, kampeni za uchaguzi zitafanyika siku saba kabla ya siku ya uchaguzi. Aidha, Kanuni zinaelekeza, kila Chama cha Siasa kinachoshiriki uchaguzi kitawasilisha ratiba yake ya mikutano ya kampeni ya uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi si chini ya siku saba kabla ya kuanza kwa kampeni.

Hivyo, kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa za Mwaka 2019 ibara 4(1-3) (Matangazo ya Serikali Na. 571, 572, 573 na 574) ya mwaka 2024, Waziri Wa Nchi, Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) Mohamed O. Mchengerwa (MB.) anautangazia umma wa Watanzania na vyama vyote vya siasavvyenye usajili wa kudumu kuwa tarehe 27 Novemba, 2024 itakuwa ni siku ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa Tanzania Bara.

Upigaji wa kura utaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa kumi kamili jioni.

BONYEZA HAPA KUTAZAMA RATIBA KAMILI YA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA WA MWAKA 2024

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA