NECTA: USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA ACSEE 2025 KUFUNGWA SEPTEMBER 30-2024

NECTA: USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA ACSEE 2025 KUFUNGWA SEPTEMBER 30-2024
NECTA: USAJILI WA WATAHINIWA WA KUJITEGEMEA ACSEE 2025 KUFUNGWA SEPTEMBER 30-2024

Katibu Mtendaji, Baraza la Mitihani la Tanzania anapenda kuwajulisha watu wote wanaotarajia kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi Mei 2025 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba;

Kipindi cha kawaida cha usajili wa Watahiniwa wa Kujitegemea kitakuwa kuanzia tarehe 01 Julai hadi 30 Septemba, 2024 kwa ada ya Shilingi 50,000/=.

Aidha, watakaojisajili kwa kuchelewa yaani kuanzia tarehe 01 Oktoba hadi 31 Oktoba, 2024 watalipa Shilingi 65,000/= na hakutakuwa na usajili mwingine baada ya tarehe 31 Octoba 2024.

Usajili utafanyika kwa njia ya mtandao (online).

Aidha, kabla ya kujisajili, waombaji wanapaswa kwenda kwenye Vituo vya Mitihani kuchukua Namba Rejea (Reference Number) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada kupitia Benki kwa kutumia ‘Control Number’.

Ufafanuzi kuhusu utaratibu na hatua za kufuata katika kutengeneza ‘Control Number’ na kujisajili, umetolewa katika tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania: Www.necta.go.tz. na kwa Wakuu wa Vituo vya Watahiniwa wa kujitegemea.

Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwani mfumo wa usajili utafungwa baada ya kipindi cha usajili kukamilika.


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA