NAFASI ZINAZOGOMBEWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024

NAFASI ZINAZOGOMBEWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024
NAFASI ZINAZOGOMBEWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Ibara 145 na 146 
inaelezea uwepo wa Serikali za Mitaa pamoja na madhumuni yake.

Mojawapo ya madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka madaraka kwa wananchi.

Aidha, Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura 287 na 
Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura 288, zinaelekeza kufanyika kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Lengo ni kuzifanya Serikali za Mitaa ziongozwe kidemokrasia.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 201A cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka za 
Wilaya) Sura 287 na Kifungu cha 87A cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka 
za Miji) Sura 288, Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ana mamlaka ya 
kutunga Kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambazo hutumika kuongoza 
uchaguzi huo.

Viongozi wanaochaguliwa katika ngazi hizi ni wenyeviti wa vijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji, wenyeviti wa mitaa, wajumbe wa kamati za mitaa na wenyeviti wa vitongoji.

Uchaguzi wa mwisho wa Serikali za Mitaa ulifanyika mwezi Novemba mwaka
2019, hivyo, uchaguzi mwingine unatakiwa kufanyika Novemba, 2024.

Uchaguzi huu unaongozwa na Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ngazi ya vijiji, Vitongoji na mitaa katika Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji, Matangazo ya Serikali Na. 571, 572 573 na 574 ya Mwaka 2024.

Kwa mujibu wa Kanuni hizi, Nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huu
ni:-

(i) Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka
za Wilaya.Kwa nafasi hizo,uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Wilaya za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 571 la Mwaka 2024).

(ii) Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo. Kwa nafasi
hiyo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Midogo za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 572 la Mwaka 2024)

(iii) Mwenyekiti wa kijiji, wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi mchanganyiko la wanaume na wanawake), wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji (kundi la wanawake) na wenyeviti wa vitongoji katika Mamlaka
za Miji. Kwa nafasi hizo, uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na.573 la Mwaka 2024) na

(iv) Mwenyekiti wa mtaa na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi Mchanganyiko la Wanaume na Wanawake) na wajumbe wa kamati ya mtaa (Kundi la Wanawake) katika Mamlaka za Miji. Kwa nafasi hizo,
uchaguzi utaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji za Mwaka 2024 (Tangazo la Serikali Na. 574 la Mwaka 2024).


Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA