NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 BUNDA DISTRICT COUNCIL

NAFASI 389 ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 BUNDA DISTRICT COUNCIL
NAFASI 389 ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 BUNDA DISTRICT COUNCIL

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serkali za Mitaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda anawatangazia Watumishi Wote wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda nafasi ya Kazi ya muda kwa ajili ya shughuli za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika tarehe 27 Novemba, 2024.

NAFASI INAYOTANGAZWA
  • Mwandikishaji wa Wapiga Kura (Nafasi 389)
MASHARTI KWA UJUMLA
  • Mwombaji lazima awe Mtumishi wa Umma (Public Servant)
  • Awe mwadilifu
  • Asiwe na dhamana au Uongozi katika Chama cha Siasa
  • Waombaji wote waambatishe nakala ya cheti cha kuzaliwa na Kitambulisho cha Uraia (NIDA) au namba ya NIDA kwa ambao hawajapata Kitambulisho.
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi (Detail CV) yenye anuani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya wadhamini watatu (Referees) wa kuaminika.
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya Elimu na Taaluma yaani nakala ya vyeti vya Kidato cha Nne au Sita pamoja na vyeti vya taaluma (Professional Certificate from respective Board, computer certificate) na picha moja ya rangi ya hivi karibuni.
  • Barua ya maombi iandikwe kwa mkono na kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza tofauti na hapo maombi hayo hayatapokelewa.
  • Kichwa cha barua ya maombi kitaje nafasi unayoomba kwa ufasaha.
  • Barua itaje cheo cha Mtumishi katika Utumishi wa UmmBarua itaje Kituo cha kazi cha mwombaji.
  • Barua ya maombi isainiwe na mwombaji mwenyewe tofauti na hivyo maombi hayo yatakataliwa.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  • Waombaji watakaokidhi sifa na vigezo watajulishwa tarehe ya usaili kupitia mbao za matangazo za Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, website ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambayo ni www.bundadc.go.tz, namba zao za simu na anuani walizotumia kwenye barua ya maombi ya kazi.
  • Watendaji wa Vijiji na Kata hawataruhusiwa kuomba nafasi hii kwa mujibu wa Kanuni ya 10 (3) ya Kanuni za Uchaguzi wa Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa Ngazi ya VIJIJI, Vitongoji na Mitaa Katika Mamlaka za Wilaya na Mamlaka za Miji za Mwaka 2024.
  • Barua za maombi ziwasilishwe kwa Mkono Masjala ya Wazi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
Barua ya maombi iandikwe kwa:
Msimamizi wa Uchaguzi,
Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, S.L.P 126,
BUNDA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 30/09/2024.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA