NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 KINONDONI MUNICIPAL COUNCIL

NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 KINONDONI MUNICIPAL COUNCIL
Karibu Nijuze Habari Blog, chanzo chako kikuu cha habari zote ndani na nje ya nchi.

Nijuze Habari Blog tumejitolea kukupa habari bora zaidi, tukitilia mkazo habari za Michezo, Ajira, Magazeti, Matokeo, Selection, Interview, Internship pamoja na Makala Mbalimbali.

NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 KINONDONI MUNICIPAL COUNCIL

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwa Mamlaka niliyopewa chini ya Kanuni 10 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji za mwaka 2024.

Tangazo la Serikali Na. 574 la tarehe 12 Septemba, 2024, ninapenda kuwatangazia Watumishi wa Umma kutuma maombi ya nafasi za kazi ya muda ya kuandikisha na kuandaa Orodha ya Wapiga Kura katika Mitaa kwa ajili ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa wa Mwaka 2024.

SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe ni Raia wa Tanzania na mwenye umri wa kuanzia miaka 18 au zaidi.
  • Awe Mtumishi wa Umma mwenye Elimu ya Kidato cha Nne au zaidi na anayejua kusoma na kuandika katika lugha ya Kiswahili na Kingereza.
  • Awe mwadilifu na mwaminifu.
  • Asiwe Mtumishi wa Umma katika Kada za Afisa Mtendaji wa Kata au Mtendaji wa Mtaa/Kijiji.
  • Asiwe Kiongozi au Kada wa Chama chochote cha Siasa.
MASHARTI YA JUMLA KWA MWOMBAJI
  • Mwombaji lazima aainishe Mtaa anaoomba kufanyia kazi.
  • Mwombaji lazima aambatishe:- (Nakala za Vyeti vya Elimu, Wasifu Binafsi (CV) unajitosheleza ukionyesha anuani ya makazi na namba za simu na Picha mbili (2) za 'Passport Size' za hivi karibuni).
  • Barua ya maombi ya kazi lazima ipitie kwa Mwajiri.
Barua ya maombi ya kazi itumwe kwa anuani ifuatayo.
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI,
S.LP 31902,
DAR ES SALAAM.

Maombi ya kazi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika Tangazo hili hayatafanyiwa kazi.

Mwisho wa kupokea Maombi ya Kazi ni tarehe 24 Septemba, 2024
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA