NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 UBUNGO MUNICIPAL COUNCIL

NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 UBUNGO MUNICIPAL COUNCIL
NAFASI ZA KAZI KUSIMAMIA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA 2024 UBUNGO MUNICIPAL COUNCIL

Msimamizi wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa mamlaka niliyopewa chini ya Kanuni ya 10 (2) ya Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa katika Mamlaka za Miji za mwaka 2024.

Napenda kuwatangazia Watumishi wa Umma kutuma maombi ya nafasi za kazi ya muda ya Kuandikisha na Kuandaa Orodha ya Wapiga Kura katika Mitaa kwa ajili ya Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Mtaa na Wajumbe wa Kamati ya Mtaa wa Mwaka 2024 Tangazo la Serikali Na. 574 la tarehe 12 Septemba, 2024.

SIFA ZA MWOMBAJI
  • Awe ni Raia wa Tanzania na wenye umri kuanzia miaka 18 au ziadi.
  • Awe Mtumishi wa Umma mwenye elimu ya Kidato cha Nne au zaidi na anaejua kusoma na kuandika katika lugha ya Kiswahili na Kingereza.
  • Awe mwadilifu na mwaminifu.
  • Asiwe Mtumishi wa Umma katika kada za Afisa mtendaji Kata na Mtendaji wa Mtaa/Kijiji.
  • Asiwe Kiongozi au Kada wa Chama chochote cha Siasa.
MASHARTI YA JUMLA KWA MWOMBAJI
  • Mwombaji lazima aanishe Mtaa anaoomba kufanyia kazi.
  • Mwombaji lazima aambatishe:-
  • Nakala za Vyeti vya Elimu.
  • Wasifu Binafsi (CV) unaojitosheleza ukionyesha anuani ya makazi na namba za simu.
  • Picha mbili (2) za "Passport Size" za hivi karibuni.
  • Barua ya maombi ya kazi lazima ipitie kwa mwajiri.
Barua ya maombi ya kazi itumwe kwa anuani ifuatayo:-
MSIMAMIZI WA UCHAGUZI,
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO,
S.L.P 55068,
DAR ES SALAAM.

Maombi ya kazi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioanishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa Kupokea Maombi ya Kazi ni tarehe 23 September, 2024
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA