NAFASI 91 ZA KAZI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

NAFASI 91 ZA KAZI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
NAFASI 91 ZA KAZI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI

✅NAFASI 87 ZA KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawatangazia Watanzania wote kuwa inazo nafasi ya Katibu Mahsusi Daraja la III (Personal Secretary III) nafasi themanini na saba (87), katika masharti ya ajira ya muda mfupi (Temporary Employment) katika Ofisi za Baraza ya Ardhi na Nyumba katika Wilaya zifuatazo;

Arumeru, Babati, Bagamoyo, Bahi, Bariadi, Bukoba, Bunda, Busega, Chato, Chemba, Dodoma, Gairo, Ifakara, Kahama, Karagwe, Karatu, Kasulu, Kibaha, Kibiti, Kibondo, Hai, Hanang', Igunga, Ikungi, Ilala, Kalambo, Kigoma, Kilindi, Kilosa, Kilwa, Kisarawe, Kishapu, Kiteto, Kongwa, Kyela, Kyerwa, Lindi, Liwale, Ludewa, Makete, Malinyi, Masasi, Maswa, Mbarali, Mbeya, Mbinga, Mbogwe, Mbulu, Meatu, Mkalama, Mkuranga, Mlele, Monduli, Morogoro, Mpanda, Mpwapwa, Mtwara, Mufindi, Muheza, Muleba, Mwanga, Mwanza, Nachingwea, Ngara, Ngorongoro, Njombe, Nkasi, Rombo, Ruangwa, Rufiji, Same, Sengerema, Serengeti, Shinyanga, Simanjiro, Songea, Mbozi, Tabora, Tandahimba, Tanganyika, Tarime, Tunduru, Ubungo, Ukerewe, Ulanga, Urambo na Wanging'ombe,

SIFA ZA WAOMBAJI:

  • Awe Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45;
  • Mkazi wa Wilaya ambayo kuna nafasi ya kazi atapewa kipaumbele;
  • Mwenye sifa na uzoefu wa kazi hii atapewa kipaumbele; na
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi pasipo kuhitaji usimamizi. (Be able to work under minimum supervision).

SIFA ZA KITAALUMA

  • Awe amehitimu kidato cha IV au VI na kufaulu;
  • Awe amehitimu Astashahada ya Mafunzo ya Uhazili kutoka kwenye Chuo cha Utumishi wa Umma (Tanzania Public Service College) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali; na
  • Awe amefaulu mtihani wa Hatua ya tatu na somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kingereza maneno 80 kwa dakika moja, pamoja na ujuzi wa kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na serikali na kupata cheti.

KAZI NA MAJUKUMU ZA KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III

  • Kuchapa nyaraka na taarifa mbalimbali za Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya zikiwemo hukumu, mienendo ya mashauri na barua;
  • Kupokea wageni na kuwasaili shida zao na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa;
  • Kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao, safari za kazi za msimamizi wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa kutekelezwa katika ofisi anapofanyia kazi na kumuarifu msimamizi wake kwa wakati unaohitajika;
  • Kuhudumia na kusimamia shughuli za uendeshaji wa Ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya;
  • Kusimamia na kuhakikisha kuwa Ofisi za Baraza zinakuwa safi na nadhifu wakati wote; na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake kwa mujibu wa Miongozo mbalimbali ya Utumishi wa Umma.

Ngazi ya Mshahara: TGS B 1

MASHARTI YA JUMLA.

  • Mwombaji awasilishe maombi katika Ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya husika;
  • Maombi yote yaambatishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV), namba za simu na anuani sahihi;
  • Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, kidato cha IV au VI, cheti cha kuzaliwa na picha mbili (2) za passport size za hivi karibuni na ziandikwe jina kwa nyuma;
  • Hati za matokeo ya kidato cha IV, VI au Chuo (Testmonial/provisional results) HAVITAKUBALIWA; na
  • Wale ambao mikataba yao inaishia tarehe 31 Agosti, 2024 wanaruhusiwa kuomba;

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 26 Septemba, 2024 saa 9:30 Alasiri.

Maombi yaelekezwe kwa anuani ifuatayo;

Katibu Mkuu,

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

S. L. P 2908,

40477 DODOMA.

------------------------------------------

NAFASI 91 ZA KAZI WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI
✅NAFASI 4 ZA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA III

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inawatangazia Watanzania wote kuwa inazo nafasi za kazi ya Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la III (Record Management Assistant III) nafasi nne (4), katika masharti ya ajira ya muda mfupi (Temporary Employment) katika Ofisi za Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya ya Kinondoni, Ilala, Lushoto na Arusha.

SIFA ZA WAOMBAJI:

  • Awe Mtanzania mwenye umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45;
  • Mkazi wa Wilaya ambayo kuna nafasi ya kazi atapewa kipaumbele;
  • Mwenye sifa na uzoefu wa kazi hii atapewa kipaumbele; na
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi pasipo kuhitaji usimamizi. (Be able to work under minimum supervision).

SIFA ZA KITAALUMA

  • Awe amehitimu kidato cha IV au VI na kufaulu;
  • Awe amehitimu Astashahada ya Mafunzo ya Utunzaji Kumbukumbu au inayohusiana na hiyo kutoka kwenye Chuo cha Utumishi wa Umma (Tanzania Public Service College) au vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali; na
  • Mwenye ujuzi wa kutumia kompyuta katika programu za Microsoft Office, Internet, Windows, E-mail na Publisher, atapewa kipaumbele.

KAZI NA MAJUKUMU ZA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA III

  • Utunzaji wa kumbukumbu za mashauri yanayosikilizwa katika Baraza; Kufungua na kuweka kumbukumbu sahihi za mashauri yanayofunguliwa katika Baraza;
  • Kuandaa na kuitisha majalada kwenda kwa Mwenyekiti kwa ajili ya usikilizaji wa mashauri;
  • Kuingia Barazani na kumsaidia Mwenyekiti katika masuala yote yanayohusiana na kumbukumbu wakati wa usikilizaji wa mashauri;
  • Kupokea risiti za malipo ya mashauri yanayofunguliwa katika Baraza; na
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na msimamizi wake kwa mujibu wa Miongozo mbalimbali ya Utumishi wa Umma.

Ngazi ya Mshahara: TGS B1

MASHARTI YA JUMLA.

  • Mwombaji awasilishe maombi katika Ofisi za Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya husika;
  • Maombi yote yaambatishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (CV), namba za simu na anuani sahihi;
  • Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, kidato cha IV au VI, cheti cha kuzaliwa na picha mbili (2) za passport size za hivi karibuni na ziandikwe jina kwa nyuma;
  • Hati za matokeo ya kidato cha IV, VI au Chuo (Testmonial/provisional results) HAVITAKUBALIWA; na
  • Wale ambao mikataba yao inaishia tarehe 31 Agosti, 2024 wanaruhusiwa kuomba;

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 26 Septemba, 2024 saa 9:30 Alasiri.

Maombi yaelekezwe kwa anuani ifuatayo;

Katibu Mkuu,

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi,

S. L. P 2908,

40477 DODOMA.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA