NAFASI 317 ZA ASKARI MGAMBO DAR ES SALAAM CITY COUNCIL

NAFASI 317 ZA ASKARI MGAMBO DAR ES SALAAM CITY COUNCIL
NAFASI 317 ZA ASKARI MGAMBO DAR ES SALAAM CITY COUNCIL

Mkurugezi wa Jiji la Dar es Salaam anawatangazia Watanzania wote wenye sifa kuomba kazi kwa nafasi zifuatazo:-

✅ASKARI MGAMBO (NAFASI - 317)

MASHARTI KWA UJUMLA:

  • Awe raia wa Tanzania
  • Awe amehitimu Kidato cha nne au sita
  • Awe na kitambulisho cha Taifa au namba ya NIDA kutoka Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa
  • Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kiingereza
  • Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibishwa na Daktari wa Serikali
  • Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya
  • Awe tayari kufanya kazi za Mgambo mahali popote ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
  • Asiwe na kumbukumbu za uhalifu
  • Awe na mafunzo ya JKT au Mgambo
  • Awe na barua ya mdhamini mwajiriwa wa Serikali na mdhamini mwananchi mwenye makazi ya kudumu ya eneo husika
  • Mwombaji hatakiwi kuwa na kosa lolote la madai au jinai
  • Awe na umri kati ya miaka 18 - 45 
  • Mwomabaji atakayewasilisha taarifa na sifa za kughushi atachukuliwa hatua za kisheria
  • Watumishi waliopunguzwa kazi/ kufukuzwa kazi/Kuachishwa kazi kwa sababu ya kughushi vyeti serikalini hawaruhusiwi kuomba.

KAZI/MAJUKUMU YA ASKARI MGAMBO

  • Kulinda mali za Soko, Operesheni na' Malindo katika Ofisi za Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaa
  • Kuhakikisha eneo analolinda linakuwa na hali ya utulivu wakati wote
  • Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na Msimamizi wa wake

Ajira ni ya mkataba wa miezi mitatu (3).

Mwajiri atalipa mshahara wa Tshs. 10,000/= [Shilingi elfu kumi tu] kwa siku yenye kuleta jumla ya 300,000/= [Shilingi laki tatu tu] kwa mwezi.

Barua zote ziambatane na nyaraka zifuatazo:

Nakala za vyeti vya mwombaji vilivyothibitishwa ambayo ni:

-Cheti cha kidato cha nne

-Cheti cha Taaluma

-Cheti cha Kuzaliwa.

-Kitambulisho cha Taifa

-Picha ndogo za rangi (colored Passport size mbili (2) za mwombaji za hivi karibuni).

Waombaji wenye sifa pungufu au zaidi na zilizotajwa hapo juu hawaruhusiwi kuomba kwani maombi yao hayatafanyiwa kazi.

Barua ambazo hazikuambatanishwa na nyaraka zilizotajwa hapo juu hazitashughulikiwa.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI:

Barua zote za maombi ziandikwe kwa mkono zikiwa na anwani kamili ya mwombaji pamoja na namba ya simu zitumwe kwa anuani ifuatayo hapa chini na zitapokelewa Karakana ya Halmashauri ya Jiji (DEPO).

Mkurugenzi wa Jiji

1 Mtaa wa Mission

S.L.P. 20950

Halmashauri ya Jiji

11883-DAR ES SALAAM

Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 18 Septemba, 2024.saa 9.30 alasiri.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA