NAFASI 2000 ZA KAZI CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA)

NAFASI 2000 ZA KAZI CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA)
Karibu Nijuze Habari Blog, chanzo chako kikuu cha habari zote ndani na nje ya nchi.

Nijuze Habari Blog tumejitolea kukupa habari bora zaidi, tukitilia mkazo habari za Michezo, Ajira, Magazeti, Matokeo, Selection, Interview, Internship pamoja na Makala Mbalimbali.

NAFASI 2000 ZA KAZI CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO (SUA)

TANGAZO LA AJIRA ZA MUDA 2000 KUPITIA PROGRAMU MAALUM YA KUENDELEZA ZAO LA PAMBA NCHINI

Chuo kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA) kinashirikiana na Wizara ya Kilimo katika utekelezaji wa programu ya kushirikisha vijana katika kilimo ya Jenga Kesho Iliyo bora (Building a Better tomorrow- BBT).

BBT inatekelezwa kupitia mikakati na miradi mbalimbali katika mnyororo wa thamani wa mazao na baadhi ya malengo yake ni kuongeza ajira kwa vijana na wanawake 20,000 kupitia shughuli za kukuza ujuzi (internship), kuanzisha shughuli za kiuchumi 12,000 katika ngazi ya vijiji pamoja na kilimo cha mashamba makubwa (Block farms) ifikapo mwaka 2030.

Kama sehemu ya mkakati wa kuimarisha huduma za ugani hapa nchini, wizara ya kilimo imepanga kutekeleza pia program maalum ya huduma za ugani kupitia vijana wahitimu (BBT Agricultural Extension Entrepreneurship Scheme- BBT AEES).

Kupitia BBT-AEES nafasi elfu mbili (2000) zinahitajika kujazwa na wahitimu wa fani za kilimo kutoa huduma za ugani katika zao la pamba kwa utaratibu wa ajira za muda kama ifuatavyo:-

✅NAFASI 1,000 ZA AFISA KILIMO

MAJUKUMU YA MUHIMU NI PAMOJA NA:

  • Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa zao la pamba kwa kufanya yafuatayo:
  • Kutoa elimu ya kilimo bora cha pamba kwa wakulima kuanzia kuandaa shamba, kuvuna hadi kuhifadhi ghalani
  • Kutoa elimu na kusimamia ubora wa pamba kuanzia shambani hadi ghalani
  • Kufuatiliia na kuhakikisha kuwa wakulima wanazingatia kanuni za kilimo bora cha pamba
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya kila wiki kuhusu maendeleao ya kilimo katika eneo husika
  • Kuandaa mahitaji ya pembejeo kwa wakulima na kuyawasilisha katika mamlaka husika
  • Kusimamia na kuhakikisha pembejeo zinazopelekwa katika eneo husika zinawafikia wakulima kikamilifu
  • Kusajili wakulima na wadau wengine ikiwemo watoa huduma za pembejeo katika eneo lake kwenye mfumo wa kidijitali uliopo
  • Kutoa mafunzo na kuanzisha vikundi vya wakulima na kuvisimamia
  • Kuanzisha mashamba ya mfano na shamba darasa katika eneo la kazi
  • Kuwatambua wadau wa sekta kilimo waliopo katika eneo la kazi na kuwaunganisha na wakulima ili kupata huduma wanazotoau
  • Kuhakikisha kila mkulima ana daftari ambalo litatumika kujaza huduma zitakazotolewa na wadau mbalimbali
  • Kukusanya, kuandaa na kuchakata takwimu za uzalishaji katika eneo lake kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji takwimu (Agricultural Routine Data System (ARDS)
  • Kusimamia matumizi ya mfumo wa kidijitali ya kutoka huduma za ugani na
  • Kutoa ushauri kwa mazao mengine yanayolimwa na wakulima wa kijiji anachokisimamia

SIFA ZINAZOHITAJIKA 

Kwa nafasi hii mwombaji awe na sifa zifuatazo:

  • Awe mtanzania mwaminifu, mweye kujituma na mahusiano mazuri na wengine
  • Awe amehitimu shahada katika fani ya sayansi ya kilimo, Agronomia au uzalishaji mazao kutoka chuo kinachotambulika na serikali
  • Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma
  • Awe hajawahi kufungwa kwa makossa yoyote ya jinai
  • Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa
  • Awe tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama itakavyoainishwa katika mkataba
  • Awe mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40
  • Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa kipindi cha msimu husika
  • Uzoefu wa kazi katika zao la pamba au ushiriki wa mafunzo ya kukuza ujuzi (internship) ndani au nje ya nchi ni sifa za ziada

✅NAFASI 1000 ZA AFISA KILIMO MSAIDIZI

MAJUKUMU YA MUHIMU NI PAMOJA NA:

Kutoa ushauri wa kitaalam kwa wakulima na wadau wengine katika mnyororo wa thamani wa zao la pamba kwa kufanya yafuatayo

  • Kutoa elimu ya kilimo bora cha pamba kwa wakulima kuanzia kuandaa shamba hadi kuvuna
  • Kutoa elimu na kusimamia ubora wa pamba kuanzia shambani hadi ghalani
  • Kufuatiliia na kuhakikisha kuwa wakulima wanazingatia kanunu za kilimo bora cha pamba
  • Kuandaa na kutoa taarifa ya kila wiki kuhusu maendeleao ya kilimo katika eneo husika
  • Kuandaa mahitaji ya pembejeo kwa wakulima na kuyawasilisha katika mamlaka husika
  • Kusimamia na kuhakikisha pembejeo zinazopelekwa katika eneo husika zinawafikia wakulima kikamilifu
  • Kusajili wakulima na wadau wengine ikiwemo watoa huduma za pembejeo katika eneo lake kwenye mfumo wa kidijitali uliopo
  • Kushiriki katika kuanzisha mashamba ya mfano na shamba darasa katika eneo la kazi
  • Kuwatambua wadau wa sekta kilimo waliopo katika eneo la kazi na kuwaunganisha na wakulima ili kupata huduma wanazotoa
  • Kufuatilia na kusimamia utunzaji na usimamizi wa daftari la mkulima ambalo litatumika kujaza huduma zitakazotolewa na wadau mbalimbali
  • Kusaidia kukusanya, kuandaa na kuchakata takwimu za uzalishaji katika eneo lake kwa kutumia mfumo wa ukusanyaji takwimu (Agricultural Routine Data System (ARDS)
  • Kushiriki kusimamia matumizi ya mfumo wa kidijitali ya kutoka huduma za ugani 

SIFA ZINAZOHITAJIKA 

Kwa nafasi hii mwombaji awe na sifa zifuatazo:

  • Awe mtanzania mwaminifu, mweye kujituma na mahusiano mazuri na wengine
  • Awe amehitimu stashahada katika fani ya sayansi ya kilimo au uzalishaji mazao kutoka chuo kinachotambulika na serikali
  • Asiwe ameajiriwa au kufukuzwa kazi katika utumishi wa umma
  • Awe hajawahi kufungwa kwa makossa yoyote ya jinai
  • Awe tayari kufanya kazi katika maeneo mbalimbali ya vijijini
  • Awe na uwezo wa kufanya kazi vizuri bila kusimamiwa
  • we tayari kufanya kazi kwa mkataba wa muda na kulipwa posho ya mwezi kama itakavyoainishwa katika mkataba
  • Awe mwenye umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 40
  • Awe tayari kusaini mkataba wa makubaliano wenye vigezo vya utendaji kazi kwa kipindi cha msimu husika
  • Uzoefu wa kazi katika zao la pamba au ushiriki wa mafunzo ya kukuza ujuzi (internship) ndani au nje ya nchi ni sifa za ziada

JINSI YA KUTUMA MAOMBI

  • Maombi yote yaambatane na vivuli vya vyeti vya kuzaliwa, NIDA, vyeti vya elimu ya sekondari, stashahada na shahada kutoka vyuo vya mafunzo vinavyotambuliwa na serikali.
  • Wahitimu watarajiwa (2024) wenye sifa tajwa hapo juu, wanahamasishwa kutuma maombi yao wakiambatanisha pia nakala za “partial transcript” au “results slips”.
  • Picha mbili za hivi karibuni za “passport size” za mwombaji
  • Wasifu (Curriculum vitae) wa mwombaji pamoja na anuani kamili, mawasiliano ya simu, barua pepe na anuani za wadhamini (referees) watatu wa kuaminika
  • Maombi yote yatumwe kwa Rasi wa ndaki ya Kilimo ya Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo kupitia barua pepe coahr@sua.ac.tz na nakala kwa mkurugenzi- kurugenzi ya Shahada za awali ya chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo dus@sua.ac.tz
Waombaji wanashauriwa kutuma maombi yao kupitia barua pepe ingawa wanaweza pia kuleta maombi moja kwa moja kwa ofisi tajwa hapo juu.

Mwisho wa kutuma Maombi

Maombi yote yawe yametufikia kabla au ifikapo tarehe 25 Septemba 2024.

Kwa maelezo zaidi au maswali juu ya tangazo hili tafadhali tupigie kupitia namba zifuatazo:

+255760485718

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA