NAFASI 20 ZA KAZI IRINGA DISTRICT COUNCIL

NAFASI 20 ZA KAZI IRINGA DISTRICT COUNCIL
NAFASI 20 ZA KAZI IRINGA DISTRICT COUNCIL

Karibu Nijuze Habari Blog, chanzo chako kikuu cha habari zote ndani na nje ya nchi.

Nijuze Habari Blog tumejitolea kukupa habari bora zaidi, tukitilia mkazo habari za Michezo, Ajira, Magazeti, Matokeo, Selection, Interview, Internship pamoja na Makala Mbalimbali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa anawatangazia Watanzania wenye  sifa na nia ya kufanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuomba nafasi za kazi  zilizotajwa hapo chini, baada ya kupokea kibali chenye Kumb Na. FA. 97/288/01/09 cha 
tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa  Umma na Utawala Bora. 

✅MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA II - (NAFASI 2) 

MAJUKUMU YA KAZI 
  • Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri;
  • Kupokea wageni na kuwasikiliza shida zao na kuwaelekeza;
  • Kutunza taarifa za kumbukumbu ya matukio, miadi, tarehe za vikao, safari za Mkuu wake  na ratiba za kazi zingine;
  • Kupokea majalada na kusambaza kwa Maofisa walio katika Idara/Kitengo/Sehemu husika;
  • Kukusanya, kutunza na kuyarejesha majalada na nyaraka sehemu zinazohusika;
  • Kupanga dondoo na kufanya maandalizi ya vikao mbalimbali;
  • Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi; na
  • Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na Mkuu wake wa kazi.
SIFA ZA KUAJIRIWA
  • Awe amehitimu Elimu ya Kidato cha Nne (IV) au Kidato cha Sita (VI)
  • Awe amehitimu mafunzo ya Stashahada (Diploma) ya Uhazili au cheti cha NTA level 6 ya Uhazili.
  • Awe amefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na Kiingereza maneno 100 kwa dakika  moja na kupata programu za kompyuta za ofisi kama vile: Word, Excel, Powerpoint,  Internet, E-mail na Publisher kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS C

✅MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III. (NAFASI 15)

MAJUKUMU YA KAZI 
  • Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji;
  • Kusimamia ulinzi na usalama wa Raia na Mali zao, kuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi  wa Utawala Bora katika Kijiji;
  • Kuratibu na kusimamia upangaji na utekelezaji wa mipango ya Maendeleo ya Kijiji;
  • Katibu wa mikutano Kamati zote za Halmashauri ya kijiji;
  • Kutafsiri na kusimamia Sera, Sheria na Taratibu;
  • Kuandaa taarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika  kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoa njaa, umaskini na kuongeza uzalishaji mali;
  • Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na Nyaraka za Kijiji;
  • Kiongozi wa wakuu wa vitengo vya kitaalam katika Kijiji;
  • Mwenyekiti wa Kikao cha Wataalam waliopo katika Kijiji;
  • Kupokea, kusikiliza na kutatua malalamiko na migogoro ya wananchi;
  • Kusimamia utungaji wa sheria Ndogo za Kijiji; na
  • Atawajibika kwa Mtendaji wa Kata.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI) aliyehitimu mafunzo ya Astashahada/ Cheti  katika moja ya fani zifuatazo:-Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha,  Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Jamii kutoka chuo cha Serikali za Mitaa au Chuo  chochote kinachotambuliwa na Serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS B

✅DEREVA DARAJA LA II NAFASI (2)

MAJUKUMU YA KAZI
  • Kuendesha Magari ya Halmashauri;
  • Kukagua gari kabla na baada ya safari ili kubaini hali ya usalama wa gari;
  • Kuwapeleka watumishi maeneo mbalimbali kwenye safari ya kikazi;
  • Kufanya matengenezo madogo madogo ya gari;
  • Kukusanya na kusambaza Nyaraka mbalimbali;
  • Kutunza na kuandika daftari ya safari (Log Book) kwa safari zote;
  • Kufanya usafi wa gari; na
  • Kufanya kazi nyingine kadri utakavyoelekezwa na msimamizi wako.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe na cheti cha Mtihani wa kidato cha nne (IV), mwenye leseni daraja “E” au “C” pamoja  na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua mwaka mmoja (1) bila  kusababisha ajali. Awe amehudhuria mafunzo ya msingi ya uendeshaji magari (basic driving course) yanayotolewa na chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) au chuo  kingine kinachotambuliWa na serikali.

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGS B

✅DEREVA WA MITAMBO DARAJA LA II NAFASI (1)

MAJUKUMU YA KAZI
  • Kuendesha mitambo kikamilifu bila kusimamiwa;
  • Kuweka vipimo mbalimbali vinavyotakiwa kufuatana na kazi anayofanya na jinsi  anavyoelekezwa na kiongozi wa kazi hiyo;
  • Kuandika vizuri ‘log sheet’ na kuweka kumbukumbu sahihi ya matumizi ya vifaa kwa mfano mafuta, grisi na vipuri;
  • Kufanya usafi wa mitambo;
  • Kuhakikisha kuwa mashine/mitambo inatumika kwa kazi zinazotakiwa; na
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na msimamizi wake.
SIFA ZA KUAJIRIWA
Awe amehitimu Elimu ya kidato cha nne (IV), mwenye leseni daraja G ya uendeshaji 
mitambo pamoja na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo. Awe na uzoefu wa  kuendesha mitambo kwa muda usiopungua saa mia tatu (300) au miezi mitatu (3) bila  kusababisha ajali. 

NGAZI YA MSHAHARA: Ngazi ya mshahara ni TGOS A

MASHARTI YA JUMLA KWA WAOMBAJI 
  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45 isipokuwa  kwa wale tu walioko kazini Serikalini; 
  • Waombaji wenye ulemavu wanahamasishwa kutuma maombi na wanapaswa  kuainisha kwenye mfumo wa kuombea ajira ulemavu walionao kwa ajili ya taarifa kwa  Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma; 
  • Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa kilichothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili; 
  • Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa  Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo. 
  • Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye  anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)  watatu wa kuaminika. 
  • Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti  vilivyothibitishwa na Mwanasheria/ Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne, Kidato  cha Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali  kwa kuzingatia sifa za kazi husika. 
  • “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati ya matokeo ya kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA. 
  • Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na  kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE). 
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa  kama wana kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi. 
  • Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika  Utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika  Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010. 
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria. 
Muhimu: Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa pamoja  na vyeti vya elimu.na anuani ya barua hiyo ielekezwe kwa; 
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, 
S.L.P. 108, 
IRINGA. 

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) 
kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’). 

Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili 
HAYATAFIKIRIWA. 

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 28/09/2024. 
DONWLOAD PDF YA TANGAZO HAPA.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA