NAFASI 18 ZA KAZI KIGOMA DISTRICT COUNCIL

NAFASI 18 ZA KAZI KIGOMA DISTRICT COUNCIL

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma anapenda kuwatangazia Watanzania  wote kuwa amepokea kibali cha kutekeleza Ajira mpya katika mwaka wa fedha 2023/2024 chenye Kumb.Na.FA.97/288/01/09 cha tarehe 25 Juni, 2024 kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais  Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Hivyo anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa  Watanzania wote wenye sifa zinazotakiwa kujaza nafasi zifuatazo:-
MASHARTI YA JUMLA
  • Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri wa kuanzia miaka18 na usiozidi miaka 45
  • Waombaji wote waambatishe maelezo binafsi yaliyojitosheleza (Detail Curriculum Vitae)  yenye anuani inayotumika, namba za simu zinazopatikana na Anuani ya Barua Pepe (E-mail  address) pamoja na majina ya wadhamini (Referees) watatu wa kuaminika.
  • Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma wapitishe barua zao za maombi ya nafasi ya  kazi kwa waajiri wao.
  • Maombi yote yaambatane na nakala ya vyeti vya Elimu na Taaluma vilivyothibitishwa na Mwanasheria/Wakili ambavyo ni vyeti vya Kidato cha Nne/Sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. 
  • Diploma/Certificates, - Cheti cha mtihani wa Kidato cha IV na VI, - Computer Certificate, - Vyeti vya Kitaaluma.
  • “Testmonial“, ‘‘Provisional Results“, “Statement of results“, hati ya matokeo ya Kidato cha Nne na Kidato cha Sita (FORM IV AND FORM VI RESULTSSLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  • Waombaji waliosoma nje ya Nchi wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na vimethibitishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA na NACTE).
  • Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wana kibali kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi.
  • Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
MUHIMU. Kumbuka kuambatanisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa na ielekezwe 
kwa anuani ya,
 Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma,
 S.L.P 332 .
 KIGOMA.

Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment
Portal) kupitia anuani ifuatayo; https://portal.ajira.go.tz/ (Anuani hii pia
inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu
iliyoandikwa 'Recruitment Portal').

Maombi yatakayowasiIishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili
HAYATAFIKIRIWA.

Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 11 Oktoba, 2024.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA