NAFASI 10 ZA KAZI KAKONKO DISTRICT COUNCIL

NAFASI 10 ZA KAZI KAKONKO DISTRICT COUNCIL

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko anayo furaha kutangaza nafasi 10 za ajira ya Vibarua kwa watanzania wote wenye sifa stahiki kwa nafasi ya Vibarua wa usafi nafasi 8 na Waingiza Taarifa katika mfumo wa TASAF MIS nafasi 2.

Nafasi za ajira hizi zinatokana na uhitaji wa Halmashauri wa huduma ya usafi na wasaidizi.

✅Vibarua wa usafi - Nafasi 8

Kazi na Majukumu
  • Kufanya usafi wa ndani
  • Kufanya usafi wa nje
  • Kuandaa kumbi za mikutano
  • Kufanya kazi nyingine kadri atakavyoelekezwa na Msimamizi wake.
Sifa za Kuajiriwa.

  • Awe anajua kusoma na kuandika
  • Muombaji awe na umri kuanzia miaka 18 na usiozidi miaka 45
  • Muombaji awe mchapakazi.
  • Muombaji awe muadilifu
✅Waingiza Taarifa kwenye mfumo wa TASAF MIS - Nafasi 2

Majukumu ya Kazi
  • Jukumu Kubwa ni Kuingiza data kwenye Mfumo TASAF MIS
  • Kuingiza taarifa za kaya (Data Update)
  • Kusajiri Miradi ya PWP
  • Kuingiza taarifa za Mahudhurio ya walengwa waliofanya kazi (mahudhurio ya kazi)
  • Kuingiza taarifa za walengwa kwa ajili ya kutimiza masharti ya Elimu na Afya Kusajili vikundi vya COMSIP
  • Kuingiza taarifa za fedha kwa wanavikundi vya kuweka akiba na kuwekeza na Uncollected
  • Kuingiza mipango kazi ya Biashara na Taarifa za malipo za walengwa Pamoja na majukumu mengine utakayopangiwa na mkuu wako wa kazi
SIFA ZA MWOMBAJI
  • Wahitimu wa kidato cha nne
  • Awe ana ujuzi wa kutumia Komputya Muombaji awe mchapakazi
  • Muombaji awe muadilifu
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 12/09/2024 saa tisa na nusu alasiri. Maombi yote yatumwe kwa kutumia anuani ifuatayo;-
Mkurugenzi Mtendaji,
Halmashauri ya Wilaya,
S.L.P. 03,
KAKONKO.

Post a Comment

Previous Post Next Post

JIUNGE NASI TELEGRAM BOFYA HAPA WHATSAPP BOFYA HAPA