MAHITAJI YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA

MAHITAJI YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA
MAHITAJI YA WANAFUNZI 3,500 WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA SEPTEMBER 2024

Vijana wote waliochaguliwa kujiunga na Jeshi la Polisi wanatakiwa kuripoti Shule ya Polisi Moshi kuanzia tarehe 30/09/2024 hadi tarehe 02/10/2024 kwaajili ya kuhudhuria mafunzo.

Aidha vijana hao wanatakiwa waripoti Shule ya Polisi Moshi wakiwa na vifaa vifuatavyo:

  • Track suti (track suit) rangi ya bluu (blue) yenye ufito mweupe, fulana (t-shirt) nyeupe isiyo na maandishi, raba, soksi nyeusi, bukta mbili (2) za bluu (blue) kwa ajili ya michezo na mazoezi pamoja na sanduku la chuma (Tranka) la rangi ya blue.
  • Chandarua cheupe cha duara na sio cha pembe nne, shuka za light blue jozi mbili (Shuka 4), blanket moja la kijivu lisilo na maua na sio duveti na pasi ya mkaa.
  • Vifaa vya usafi: reki, jembe lenye mpini, panga, ndoo mbili ndogona fagio la chelewa.
  • Kadi ya bima ya Afya (NHIF) au fedha taslimu Tsh. 50,400/= kwa wasio na kadi za bima ya Afya.
  • Vyeti halisi vya taaluma (Original Academic Certificates), cheti halisi cha kuzaliwa, kadi ya NIDA au namba ya Utambulisho wa Taifa (NIDA), Nakala za kadi za NIDA au namba za Utambulisho wa Taifa (NIDA) za wazazi na watu wa karibu upande wa Baba na Mama (kama vile Baba Mkubwa, Mdogo, Shangazi, Mama mkubwa, mdogo, mjomba, Babu, Bibi nk) passport size 06 (background blue), na nakala (copy) 5 kwa kila cheti kilichoainishwa hapo juu.
  • Fedha ya kujikimu.
  • Simu za mkononi haziruhusiwi chuoni, hivyo ni marufuku kuripoti Shule ya Polisi Moshi na simu ya mkononi.
  • Yeyote atakaepatikana na simu itachukuliwa kuwa ni utovu wa nidhamu na adhabu yake ni kufukuzwa mafunzo mara moja.
  • Shule itaelekeza utaratibu wa kupata mawasiliano. 
Kwa yeyote atakaye ripoti Shule ya Polisi Moshi baada ya tarehe 02/10/2024 hatopokelewa na atahesabika amejiondoa mwenyewe kwenye mafunzo. 

DONWLOAD PDF MAJINA YA VIJANA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI TANZANIA KATIKA SHULE YA POLISI MOSHI 2024.

Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA