JINSI YA KUTUMA MAOMBI JESHI LA JWTZ

Karibu Nijuze Habari Blog, chanzo chako kikuu cha habari zote ndani na nje ya nchi.

Nijuze Habari Blog tumejitolea kukupa habari bora zaidi, tukitilia mkazo habari za Michezo, Ajira, Magazeti, Matokeo, Selection, Interview, Internship pamoja na Makala Mbalimbali.

JINSI YA KUTUMA MAOMBI JESHI LA JWTZ
July 30-2024 Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania JWTZ Limetangaza nafasi za kuandikishwa Jeshini kwa vijana wa kitanzania wenye Elimu ya kidato cha nne na kidato cha sita.

Kupitia Makala hii utaweza kuona Jinsi ya Kutuma Maombi Jeshi hilo pamoja mahitaji yote.

Aidha, uandikishaji utahusisha vijana waliopo katika makambi ya Jeshi la Kujenga Taifa 'Operesheni Jenerali Venance Mabeyo' na waliomaliza mkataba ambao wamefanya mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria na kwa Mkataba wa kujitolea.

✅SIFA ZA MWOMBAJI (VIJANA
WALIOMALIZA MKATABA WA JKT)
WALIOPO NA JKT.

Vijana wenye nia ya kuandikishwa Jeshi wanatakiwa kuwa na
sifa zifuatazo:-

  • Awe raia wa Tanzania.
  • Awe na umri usiozidi miaka 25.
  • Awe na afya nzuri na akili timamu.
  • Mwenye tabia na nidhamu nzuri, hajapatikana na hatia ya makosa ya jinai mahakamani na kufungwa.
  • Awe na cheti halisi cha kuzaliwaAwe na vyeti vya shule.
  • Awe hajatumikia Jeshi la Polisi, Magereza, Chuo cha Mafunzo au Kikosi Maalumu cha kuzuia Magendo.
  • Awe amehitimu mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mkataba wa kujitolea miaka miwili (2) au mafunzo ya Mujibu wa Sheria na kutunukiwa cheti.

✅UTARATIBU WA KUTUMA MAOMBI
Utaratibu wa kutuma maombi ni ifuatavyo:-

  • Kwa vijana waliopo katika makambi ya JKT 'Operesheni Jenerali Venance Mabeyo' taratibu zao zinaratibiwa na Makao Makuu ya Jeshi.
  • Kwa vijana waliopo nje ya Makambi ya JKT, maombi yao yaandikwe kwa mkono na kuwasilishwa Makao Makuu ya Jeshi Dodoma kuanzia tarehe 01 Agosti, 2024 hadi tarehe 14 Agosti, 2024 yakiwa na viambatisho vifuatavyo:-
  • Nakala ya kitambusho cha Taifa au namba ya NIDA.
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Nakala za vyeti vya Shule.
  • Nakala ya cheti cha JKT.
  • Nambari ya simu ya mkononi ya mwombaji.

MAOMBI YATUMWE KWA ANUANI IFUATAYO
Mkuu wa Utumishi Jeshini,
Makao Makuu ya Jeshi,
Sanduku la Posta 194,
DODOMA, Tanzania

Utaratibu wa kujiunga na JWTZ

Uandikishaji

Mtu yeyote ataandikishwa kujiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa sifa zifuatazo: -

  • Awe raia wa Tanzania
  • Awe na Elimu ya kidato cha nne na kuendelea na awe amefaulu..
  • Awe hajaoa/hajaolewa
  • Awe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25
  • Awe na tabia na mwenendo mzuri
  • Awe na akili timamu na afya nzuri

Masharti ya Utumishi

Askari atapewa nambari ya utumishi baada ya kufaulu mafunzo ya awali.

Atalitumikia Jeshi kwa kipindi cha mwanzo cha miaka sita, baada ya hapo atafanya kazi kwa mkataba wa miaka miwili miwili kwa kibali cha Mkuu wa Majeshi.

Maafisa

Bodi ya Uteuzi wa Maafisa (Officers Selection Board)
huwafanyia usaili Askari wenye elimu ya kidato cha sita na kuendelea toka Vikosini na Shule za Askari wapya (Recruitment Schools).

Watakaofaulu masailiano hayo hupewa hadhi ya Afisa Mwanafunzi (Officer Cadet), na hupelekwa Chuoni (Tanzania Military Academy) kwa mafunzo ya Uafisa kwa muda wa mwaka mmoja.

MAJUKUMU YA MSINGI YA JWTZ

  • Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
  • Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
  • Kufanya mafunzo na mazoezi, ili kujiweka tayari kivita wakati wote;
  • Kufundisha Umma shughuli za ulinzi wa Taifa;
  • Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa;
  • Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT); na
  • Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.

MGAWANYO WA JWTZ

JWTZ inaundwa na sehemu kuu tano. Mgawanyiko huu unatokana na majukumu na mahitaji ya kiulinzi yafuatayo:-

MAKAO MAKUU YA JESHI

Makao Makuu ya Jeshi inalo jukumu kubwa la mipango ya kimkakati pamoja na uamrishaji.

KAMANDI YA JESHI LA NCHI KAVU

Kamandi hii ilianzishwa mnamo tarehe 25 Disemba, 2007 na kuzinduliwa rasmi na aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne, Mheshimiwa Dkt Jakaya Mrisho Kikwete tarehe 04 Machi, 2009.

Kuanzishwa kwa Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kumetokana na dhamira safi ya viongozi wa Serikali na Makamanda kuona umuhimu wa kuwa na kamandi ya Jeshi la nchi Kavu ili kusimamia majukumu ya kiutendaji na kiutawala.

Majukumu ya Kamandi

  • Kuimarisha usalama wa mipaka ya nchi kwa kushirikiana na kamandi zingine;
  • Kutoa mafunzo bora kwa Jeshi la Nchi Kavu;
  • Kuwaandaa maafisa na Askari wa JWTZ;
  • Kuwaandaa Maafisa na Askari kwa kuwajengea uwezo wa kufanya kazi na Kamandi zingine wakati wa vita;
  • Kusaidia Mamlaka za kiraia katika kukabiliana na maafa pindi yanapotokea;
  • Kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa Ulinzi na Usalama wa nchi na mipaka ya nchi dhidi ya adui yeyote wa ndani na wa nje; na
  • Kuandaa maafisa na Askari wanaoshiriki katika ulinzi wa Amani;

KAMANDI YA JESHI LA ANGA

Kamandi ya Jeshi la Anga ni moja ya Kamandi muhimu zinazounda Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania, kiutendaji, kivita na kiutawala na ilianzishwa mwaka 1982. Kamandi ya Jeshi la Anga inayo majukumu ya ziada ya msingi katika kutimiza wajibu wake wa ulinzi wa Anga la Tanzania. Kamandi hiyo hiyo inao uzoefu katika kusafirisha maafisa na Askari wakati wa Amani na dharuara, pia husaidia mamlaka za kiraia kutimiza wajibu wake.

Majukumu ya Kamandi ya Jeshi la Anga

  • Kutoa ulinzi wa Anga kwa maeneo muhimu ya kitaifa;
  • Kutoa ulinzi wa Anga kwa maeneo na vituo muhimu vya kijeshi
  • Kutoa msaada wa kimapigano kwa Operesheni za Majeshi ya Nchi Kavu na wanamaji;
  • Kutoa msaada kwa Mamlaka za kiraia hasa nyakati za maafa ya kitaifa na kusindikiza ndege za viongozi pia hukusanya taarifa za kiusalama;
  • Kuendeleza juhudi za mahusiano ya kijeshi na nchi nyingine kwa njia ya mazoezi ya pamoja na kushiriki katika Operesheni za umoja wa Mataifa.

KAMANDI YA JESHI LA WANAMAJI

Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ni moja ya Kamandi zinazounda Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. Kamandi hii ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 06 Disemba, 1971 wakati wa Awamu ya Kwanza wa Ujenzi wa Jeshi la kisasa lililokuwa na mtizamo wa kizalendo wa kuwalinda wananchi. Kuanzishwa kwa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ilikuwa ni jambo la muhimu la kimkakati kwa ajili ya kuendelea kuhakikisha kuwa mipaka yote inakuwa salama. Baadhi ya Madhumuni ya kuanzishwa kwa Kamandi ya Jeshi la Wanamaji ni yafuatayo:-

  • Kukamilisha Muundo wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa kuwa kila nchi yenye bahari, maziwa na mito mikubwa inahitaji kuwa na Kamandi ya Wanamaji, ili kusimamia ulinzi wa maeneo hayo;
  • Kuhakikisha mipaka yote katika bahari, maziwa na mito mikubwa inakuwa salama wakati wote; na
  • Kuwapa ulinzi wa kutosha wananchi wanaoishi kwa kujishughulisha na uvuvi baharini, maziwa na mito mikubwa,ili waweze kujipatia kipato chao na kuinua uchumi wa Taifa.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA