Kupitia Makala hii utaweza kuelewa namna ya kupata namba yako ya NIDA kwa njia ya mtandao endapo utakua umeisahau au unataka kujua kama imetoka baada ya Kujisajili kwenye Ofisi za NIDA Wilayani kwako.

Namba ya NIDA ni namba muhimu hapa nchi kwani imekua kama lazima ili uweze kupata huduma mbali mbali.

Ukiwa hauna namba ya NIDA huwezi kusajili kupata namba ya simu/laini, huwezi kufungua account bank, kwa ufupi ni huduma zote za kiserikali na zengine nyingi ambazo bila kitambulisho cha Taifa (NIDA) au

Kama umesahau namba yako ya nida unaweza pata kwa kujaza taarifa zako chache kupitia link hii hapa chini.

Jaza taarifa zako zilizoorodheshwa hapa chini kwa usahihi ili kufahamu namba yako ya Utambulisho (Namba ya NIDA)

Jina la Kwanza (Firstname)

Jina la Mwisho (Surname)

Tarehe ya Kuzaliwa

DD-MM-YYYY

Jina la kwanza la Mama

Jina la Mwisho la Mama

Taarifa hizo juu zinapaswa kufanana na zile ulizozijaza wakati unajiandikisha Kupata namba ya NIDA.

Aidha watu wengi wamekuwa wakishindwa kupata namba zao za NIDA kwa kujaza taarifa tofauti na zile za awali, hii inatokana na kujaziwa wakati wa usajili hivo kupelekea kukosea spelling za majina au tarehe za kuzaliwa.

Hivo basi tunawashauri kujaza taarifa zenu wenyewe au kutoa Copy na kuitunza Ile fomu uliyoijaza Kwa Mtendaji kabla ya kuikabidhi NIDA.

Hii itasaidia siku una uhitaji na hiyo namba na umeisahau unatoa Ile fomu unaangalizia taarifa zako jinsi zilivyo ndivyo unavyojaza na unapata namba yako na kuendelea na huduma.

BONYEZA HAPA KUANGALIA NAMBA YAKO YA NIDA.