JINSI WA KUANDIKA BARUA YA KUOMBA KAZI KUPITIA AJIRA PORTAL

JINSI WA KUANDIKA BARUA YA KUOMBA KAZI KUPITIA AJIRA PORTAL
JINSI WA KUANDIKA BARUA YA KUOMBA KAZI KUPITIA AJIRA PORTAL

Kuandika barua ya kuomba kazi ni hatua muhimu katika hatua za kuomba ajira mbalimbali .

Kwa kuwa barua yako ni sehemu muhimu ya maombi yako, basi inapaswa kuwa ya kuvutia na yenye maelezo sahihi ili kumrisha mwajiri.

Hapa chini tumekuwekea mwongozo wa hatua kwa hatua jinsi ya kuandika barua ya kuomba kazi kupitia Ajira Portal (PSRS).

Mara baada ya kufungua Ajira Portal, hakikisha unajua ni wapi unahitaji kuweka taarifa zako.

Hii itajumuisha jina lako, anuani, na taarifa nyingine muhimu, hakikisha umejaza sehemu hizi kwa usahihi.

Barua yako ya kuomba kazi inapaswa kuanza na vichwa vya habari.
- Jina lako kamili
- Anuani yako ya posta
- Nambari ya simu
- Anuani ya barua pepe
- Tarehe

Baada ya taarifa zako, andika anuani ya mpokeaji ikiwa unayo na ikiwa una majina ya watu au idara maalum, tafadhali weka hapa.

Utangulizi
Katika sehemu hii, utajitambulisha mwenyewe na kueleza sababu ya kuandika barua hiyo.

Unaweza kusema:
Naitwa Jina lako kamili na ninapenda kuwasilisha maombi yangu ya kazi kwa nafasi ya Jina la Nafasi] iliyo tangazwa kwenye Ajira Portal."

Baada ya hilo, elezea uzoefu wako na elimu kwa ufupi. Eleza jinsi uzoefu wako na elimu yako inavyokufaa kuajiriwa katika nafasi hiyo unayoiomba:

Nina uzoefu wa miaka idadi katika sehemu ya kazi na nimehitimu kwa digrii/cheti kutoka jina la taasisi. Katika nafasi yangu ya awali, nilikuwa na jukumu la elezea majukumu yako.

Sifa na Uwezo wako.
Fafanua sifa na uwezo wako wa kipekee. Andika kuhusu ujuzi maalum, mafanikio ya kazi, au mradi uliokamilisha kwa mafanikio:

Nina ujuzi mzuri katika sehemu ya ujuzi na nimeweza kufanikisha mfano wa mafanikio. Hii itaniwezesha kutoa mchango mkubwa katika nafasi hii.

Mwisho
Funga barua yako kwa ombi la kufanyiwa mahojiano.

Sisitiza nia yako ya kushirikiana na waajiri wako na kuwa na matumaini ya kusikia kutoka kwao hivi karibuni:

Ningependa kuwa na fursa ya kujadili jinsi ninavyoweza kuchangia kwa mafanikio ya jina la kampuni.

Nitarajia kusikia kutoka kwenu hivi karibuni. Asante kwa kuzingatia maombi yangu.

Saini/sahihi
Mwisho wa barua yako, weka jina lako kamili na sahihi yako kama unatumia barua ya kimkakati.

Katika Ajira Portal, unaweza kuwa na sehemu ya kuandika saini yako kwa njia ya mtandao.

Zingatia:
Hakikisha barua yako haina makosa ya lugha.
Fanya Utafiti ili uifahamu kampuni na nafasi unayoiomba kabla ya kuandika barua yako na
Tumia lugha rahisi na yenye kueleweka.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA