Karibu Nijuze Habari Blog, chanzo chako kikuu cha habari zote ndani na nje ya nchi.
Kiungo Mshambuliaji , Feisal Salum Abdallah amepiga chini ofa ya pili ya Azam FC iliyomtaka kuongeza mkataba mpya.
Feisal Salum anatajwa kuhitaji changamoto mpya ndani au nje ya nchi.
Baada ya kugoma kuongeza Mkataba pale Azam FC, Klabu hiyo imetajwa kuwa kuandaa ofa nyingine ili kumbakisha Feisal.
Aidha inatajwa kuwa viongozi wa Simba walifanya mazungumzo na Feisal zaidi ya mara mbili na dili hilo halikufanikiwa kukamilika.
Kwa sasa ni Yanga ambao wanafuatilia kwa ukaribu maendeleo ya Feisal pale Azam FC huku wakiamini Mzanzibar huyo anaweza kurejeshwa tena jangwani mwishoni mwa msimu huu wa 2024/2025.
Kutokana na hayo ni wazi tutarajie kumuona Feisal Salum katika vilabu vya Simba au Yanga msimu ujao wa 2025/2026.