BEI Mpya za Mafuta Tanzania September 2024

BEI Mpya za Mafuta Tanzania September 2024

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia Jumatano ya tarehe 4 Septemba 2024 saa 6:01 usiku. Kwa mwezi Septemba 2024, bei za rejareja na za jumla katika Mikoa ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara ni kama zinavyoonekana katika Jedwali Na. 1 na 2, mtawalia.
Bei za mafuta za rejareja kwa maeneo mbalimbali ya miji, wilaya na mikoa ni kama zinavyooneshwa katika Jedwali Na. 3.

MWENENDO WA BEI ZA MAFUTA KATIKA SOKO LA DUNIA 

Bidhaa za mafuta zinazoagizwa na kupokelewa nchini zinazingatia bei za mafuta yaliyosafishwa (FOB) kutoka soko la Uarabuni.

Mwezi Septemba 2024, bei kikomo za mafuta zimekokotolewa kwa kuzingatia bei za soko la Uarabuni za mwezi Agosti 2024.

Kwa kulinganisha na bei za Julai 2024, bei za Agosti 2024 za petroli, dizeli na mafuta ya taa zimepungua kwa wastani wa 7.68%, 6.22% na 6.20%, mtawalia.

MWENENDO WA GHARAMA ZA UAGIZAJI 
Gharama za uagizaji wa mafuta (premiums) zimepungua kwa wastani wa 10.55% kwa petroli na 13.64% kwa dizeli na kuongezeka kwa 3.37% kwa mafuta ya taa katika Bandari ya Dar es Salaam; zimepungua kwa wastani wa 4.46% kwa petroli na dizeli katika Bandari ya Tanga; na zimepungua kwa wastani wa 14.98% kwa mafuta ya petroli na dizeli katika 
Bandari ya Mtwara.

VIWANGO VYA KUBADILISHA FEDHA ZA KIGENI
Gharama za mafuta yanayopokelewa (FOB) na gharama za uagizaji (premiums) hulipiwa kwa kutumia fedha za kigeni ikiwemo Dola ya Marekani.

Kwa bei za mwezi Septemba 2024, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni (Applicable Exchange Rate) umepungua kwa 0.91%. Wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa rejareja wanatakiwa 
kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika Jedwali Na. 3.

Aidha, wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla wanatakiwa kuuza mafuta kwa bei zinazooneshwa katika 
Jedwali Na. 2. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mfanyabiashara yoyote atakayekiuka AGIZO hili.

EWURA inapenda kuwakumbusha wafanyabiashara wa bidhaa za mafuta kwa jumla na rejareja pamoja na jamii kuzingatia yafuatayo: -

  • bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli kwa eneo husika zinapatikana kupitia simu za mkononi kwa kupiga namba *152*00# na kisha kufuata maelekezo.
  • Huduma hii ni bure na inapatikana kupitia mitandao yote ya simu za mkononi hapa nchini.
  • Kwa mujibu wa Sheria ya Mafuta ya mwaka 2015, kifungu namba 166, bei za bidhaa za mafuta ya petroli zitaendelea kupangwa na soko. EWURA itaendelea kuhamasisha ushindani kwa kutoa taarifa za bei kikomo za bidhaa za mafuta.
  • Kampuni za mafuta ziko huru kuuza bidhaa za mafuta ya petroli kwa bei ya ushindani isipokuwa bei hizo zisizidi bei kikomo (Price cap) au kuwa chini ya bei iliyoruhusiwa (Floor Price) kama zilivyokokotolewa kwa mujibu wa Kanuni za EWURA za Kupanga Bei za Mafuta za Mwaka 2022 zilizotangazwa tarehe 28 Januari 2022 kupitia Gazeti la Serikali Na. 57 na marekebisho ya Kanuni tajwa kupitia Gazeti la Serikali Na. 761A la tarehe 30 Oktoba 2023 na Mabadiliko ya Kanuni za Uagizaji wa Mafuta kwa Pamoja za Mwaka 2024.
  • Vituo vyote vya mafuta vinatakiwa kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei za mafuta, punguzo, vivutio vya kibiashara vinavyotolewa na kituo husika.
  • Pale ambapo inawezekana kuchagua, wateja wanashauriwa kununua bidhaa za mafuta katika vituo vinavyouza mafuta kwa bei nafuu zaidi ili kushamirisha ushindani.
  • Wateja wanaweza kutoa taarifa za kituo chochote kinachouza mafuta juu ya bei kikomo kwa kupiga simu ya bure namba 0800110030 au kwa kuwasilisha kwa maandishi kupitia Ofisi za EWURA au kwa kutuma baruapepe kupitia info@ewura.go.tz.
  • Ni kosa kuuza mafuta bila kuweka mabango ya bei inayoonekana vizuri kwa wateja.
  • Adhabu kali itatolewa kwa kituo husika kwa kutotekeleza matakwa ya kisheria kwa mujibu wa kanuni husika.
  • Wauzaji wa bidhaa za mafuta ya petroli wanatakiwa kutoa stakabadhi za mauzo kutoka kwenye Electronic Fiscal Pump Printers (EFPP) na wanunuzi wahakikishe wanapata stakabadhi hizo za malipo zinazoonyesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. 
  • Stakabadhi hizo zitatumika kama kidhibiti kwa wanunuzi wa mafuta endapo kutajitokeza malalamiko ya kuuziwa mafuta kwa bei ya juu kuliko bei kikomo au kuuziwa mafuta yasiyo na kiwango cha ubora unaotakiwa. Stakabadhi hizo pia zitasaidia kurahisisha ukusanyaji wa kodi za Serikali zitokanazo na mauzo ya bidhaa za mafuta ya petroli.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA