Huduma hii ya LIPA kwa Simu imekuja ili kuboresha mazingira ya Wafanyabiashara na Makampuni kwa kupanua mbinu za malipo kutoka kwa wafanyabiashara na Makampuni na Wauzaji wa aina mbalimbali.
Mawakala wa jumla na rejareja wataweza kununua na kulipia bidhaaa zao kwa kutumia huduma hii ya LIPA KWA M-PESA au LIPA KWA SIMU, Njia hii ni ya haraka, salama na inampa mteja wepesi zaidi wa kufanya biashara.
Mfanyabiashara atakuwa na Lipa namba na QR code ambazo zitaruhusu wateja kulipia bidhaa kwa kuingiza Lipa namba au kuskani picha ya QR.
Lipa Kwa Simu imewawezesha wateja wa mitandao na benki zote kufikia malipo kwa urahisi, usalama ukilinganisha na fedha taslimu ambazo ni za gharama na hatari ndiyo maana tunasema M-Pesa nyumbani kwa malipo ya kidijitali.
Kwa kutumia msimbo wa QR ulioboreshwa ambao hurahisisha matumizi ya malipo zaidi kwa kuondoa hitaji la kuandika hadi nambari katika sehemu za kugusa rejareja.
Lipa Kwa Simu inaweza kutumika katika maduka mbalimbali katika mtaa wako k.m. migahawa, maduka ya rejareja, vituo vya mafuta, saluni, baa, maduka makubwa, maduka ya vifaa vya ujenzi, maduka ya dawa na maduka mengine yoyote.
Kwa msaada piga 100/101, WhatsApp 0754100100 au tuma barua pepe kwa support@vodacom.co.tz
Jinsi ya Kutumia Kwa Wateja wa Vodacom
Kwenye USSD
Piga *150*00#
Chagua 4 (Lipa kwa M-pesa)
Chagua 1 ( Lipa kwa Simu)
Ingiza Lipa Namba
Ingiza LIPA Namba
Ingiza kiasi cha kulipa
Ingiza namba ya Siri kuthibitisha
Jinsi ya Kutumia Kwa Wateja wa Tigo
Piga *150*00#
Chagua kutuma pesa
Chagua kwa mitandao mingine
Chagua M-Pesa
Weka nambari ya Lipa (tarakimu sita au saba)
Weka kiasi kwa Tshs na pini
Utapokea SMS ili kuthibitisha muamala.
Jinsi ya Kutumia Kwa Wateja wa Halotel
Piga *150*88#
Chagua kutuma pesa
Chagua kwa mitandao mingine
Chagua M-Pesa
Weka nambari ya Lipa (tarakimu saba)
Weka kiasi kwa Tshs na pini
Utapokea SMS ili kuthibitisha muamala.
Jinsi ya Kutumia Kwa Wateja wa Zantel
Piga *150*02#
Chagua kutuma pesa
Chagua kwa mitandao mingine
Chagua M-Pesa
Weka nambari ya Lipa (tarakimu sabaWeka kiasi kwa Tshs na pini
Utapokea SMS ili kuthibitisha muamala.
Jinsi ya Kutumia Kwa Wateja wa Airtel
Piga *150*60#
Chagua kutuma pesa
Chagua kwa mitandao mingine
Chagua M-Pesa
Weka nambari ya Lipa (tarakimu saba)
Weka kiasi kwa Tshs na pini
Utapokea SMS ili kuthibitisha muamala.
ADA za Lipa Kwa M-pesa (Lipa kwa Simu)
Jinsi ya Kulipa Wafanyabiashara: Kulipa kutoka kwa akaunti za Benki
Fungua menyu ya huduma ya kifedha ya benki yakChagua malipo
Chagua lipa na
Chagua Lipa kwa M-Pes
Weka nambari ya Lipa (tarakimu sita au saba)
Weka kiasi kwa Tshs ikifuatiwa na Pin yako ya benki
Utapokea SMS ili kuthibitisha muamala.
Unapofanya malipo kwa wafanyabiashara waliosajiliwa katika huduma ya LIPA KWA M-PESA utatozwa ada ndogo ya 0.5% ya kiasi unacholipa kwa malipo yote ya hadi Tsh 1,500,000/=.
Kwa msaada zaidi wasiliana na huduma kwa wateja kwa kupiga namba 100 bure.
BOFYA HAPA KUDOWNLOAD PDF
Amount From (Tsh) | Amount To (Tsh) | Fees (Tsh) |
---|---|---|
100 | 999 | 20 |
1,000 | 1,999 | 50 |
2,000 | 2,999 | 70 |
3,000 | 3,999 | 100 |
4,000 | 4,999 | 200 |
5,000 | 6,999 | 300 |
7,000 | 9,999 | 500 |
10,000 | 14,999 | 500 |
15,000 | 19,999 | 850 |
20,000 | 29,999 | 920 |
30,000 | 39,999 | 1,000 |
40,000 | 49,999 | 1,200 |
50,000 | 99,999 | 1,700 |
100,000 | 199,999 | 2,000 |
200,000 | 299,999 | 2,600 |
300,000 | 399,999 | 3,000 |
400,000 | 499,999 | 3,300 |
500,000 | 599,999 | 4,500 |
600,000 | 699,999 | 5,500 |
700,000 | 799,999 | 5,700 |
800,000 | 899,999 | 6,000 |
900,000 | 1,000,000 | 6,000 |
1,000,001 | 3,000,000 | 6,000 |
3,000,001 | 10,000,000 | 6,000 |
Ikiwa unahitaji Lipa number kwaajili ya Biashara yako tutumie ujumbe WhatsApp namba +255756658100.
Lipa number tunatengeneza Bure