820 WAITWA KWENYE USAILI SONGWE DISTRICT COUNCIL

820 WAITWA KWENYE USAILI SONGWE DISTRICT COUNCIL
MAJINA 820 YA WALIOITWA KWENYE USAILI HALMASHAURI YA WILAYA YA SONGWE 20-09-2024

Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Songwe anapenda kuwataarifu Waombaji Kazi wote walioomba kazi kuwa usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 26/09/2024 hadi 30/09/2024 na
hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.

Wasailiwa wanaoitwa kwenye
usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
  • Usaili utafanyika kuanzia tarehe kama ilivyooneshwa kwenye tangazo hili muda na sehemu ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada.
  • Kila msailiwa anatakiwa kufika kwenye eneo la usaili akiwa amevaa Mavazi nadhifu.
  • Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi; 
  • Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpiga kura, Kitambulisho cha Uraia, Hati ya kusafiria, Leseni ya Udereva au Barua ya Utambulisho toka kwa Mtendaji wa Kijiji/ Mtaa.
  • Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Astashahada na Stashahada, kutegemeana na sifa za Mwombaji.
  • Kwa upande wa Madereva hakikisha unakuja na Leseni iliyo hai.
  • Wasailiwa watakaowasilisha Testimonials, Provisional Results, Statement of results, hati za matokeo za Kidato cha IV na VI (form V and form VI results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI.
  • Kila msailiwa atajigharamia kwa Chakula, Usafiri na Malazi.
  • Kila Msailiwa azingatie tarehe, muda na mahali usaili utakapofanyika.
  • Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (kama TCU, NACTE au NECTA).
  • Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji ya tangazo husika.
  • Wasailiwa wote walioitwa kwenye usaili wahakikishe wanaingia kwenye akaunti zao na kunakili namba ya mtihani kwa kuwa namba hizo hazitatolewa siku ya usaili.
  • Hali ya hewa ya Mkwajuni Makao Makuu ya Wilaya ya Songwe ni Joto hivyo Wasailiwa wanashauriwa kuwa na nguo za aina zote nguo za Baridi kwa Mazingira ya njiani na nguo za Joto kwa Mazingira ya Mkwajuni.
  • Namna ya kufika Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, kwa wanotokea Barabara ya Makambako Mbeya utashuka Mbeya Mjini, utapanda daladala ya kwenda Mbalizi ukifika Mbalizi ulizia Magari yanayokwenda Mkwajuni.
  • Kwa wanaotokea njia ya Sumbawanga utashuka Mbalizi halafu utapanda Magari yanayokwenda Mkwajuni, Kituo cha kushukia ni Halmashauri.
Post a Comment (0)
Previous Post Next Post

PATA NYIMBO ZOTE MPYA BONYEZA HAPA

 

MATANGAZO YA BIASHARA WASILIANA NASI KUPITIA nijuzehabariblog@gmail.com

 

JIUNGE NA GROUP ZETU HAPA CHINI UPATE FURSA KAMA HIZI KILA SIKU.

 

GROUP LA WHATSAPP NO 1 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 2 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 3 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 4 BOFYA HAPA

 

GROUP LA WHATSAPP NO 5 BOFYA HAPA